Thursday, May 12, 2016

RAIS WA BRAZILI ATUMBULIWA JIPU

Mtu wangu kama utakuwa karibu na vyombo vya habari vya kimataifa story inayochukua headline sasa hivi ni kuhusu aliyekuwa Rais wa Brazil wa kwanza mwanamke Dilma Rousself kusimamishwa kazi ya urais. Hatua hiyo imekuja baada ya Bunge la Seneti Brazil kupiga kura kuidhinisha kutokuwa na imani na kiongozi huyo wa Taifa ambapo amesimamishwa kwa siku zisizozidi 180 wakati bunge hilo likichunguza tuhuma za rushwa zinazomkabili. Masenata 55 waliunga kuidhinishwa kura hiyo ya kutokuwa na iman na 22 walipinga.

MTOTO Wa CHACHA WANGWE AFIKISHWA MAHAKAMANI

BOB Chacha Wangwe (24), mtoto wa mwanasiasa marehemu Chacha Wangwe, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii anaandika Faki Sosi.Akisoma kesi hiyo namba 167, Paul Kagoshi mbele ya Waliarandwe Rema, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo amesema kuwa, Bob Chacha Wangwe amefikishwa mahakamani hapo kwa kutenda kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake Facebook.Mshitakiwa anadaiwa kutenda hayo tarehe 15 Machi na kwamba alichapicha maneno haya Tanzania ni ambayo….inajaza chuki wananchi … matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania bara kwa sababu za kijinga.Mtuhumiwa amekiri kutenda makosa hayo hivyo amerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 17 Mei mwaka huu.

Monday, May 9, 2016

Wajue wafanya biashara wakubwa Wa sukari tanzania

mstakabali wa sukari na hatima ya viwanda vya sukari nchini. Sukari yote nchini inayoagizwa kutoka nje kwa kiasi kikubwa ilikuwa inaagizwa na hawa matajiri wakubwa nchini kama wanavyoonekana kwenye picha. Hawa ni baadhi ya matajiri ambao wanamiliki soko la sukari nchini ambalo wakati wa utawala wa Rais Kikwete, hakuweza kuwadhibiti ili kuvilinda viwanda vya sukari nchini na afya za walaji. Hawa kwenye picha hapo chini ni aina ya watu wanaoitwa sugar industries movers and shakers katika jumuiya ya wafanyabiashara nchini. Kutoka kushoto ni Harun Daudi Zakaria ambaye juzi vikosi vya usalama nchini vilikuta kwenye magodauni yake huko Mbagala na Tabata tani zaidi ya 4,600 ambazo inasemakana zilikuwa zimefichwa, kwa lugha ya kisheria wanasema hoarding commodities. Huyu wakati mwingine alikuwa anapewa vibali ambavyo waingereza wanasema special/exclusive permit kununua au kuagiza sukari kwa ajili ya soko la Zanzibar. Anayefuatia ni Said Salim Bakhresa ambaye hununua sukari nchini au kuagiza nje ya nchi maelfu ya tani za sukari kama malighafi kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa kwenye viwanda vyake. Anayefuatia ni Reginald Mengi ambaye ana viwanda vya vinywaji. Hununua sukari nchini au kuagiza nje ya nchi maelfu ya tani kama malighafi kwa ajili ya viwanda vyake mbali mbali. Anayefuata ni Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ambaye baada ya kushindwa vita ya sukari kutokana na nguvu kubwa waliyonayo hawa wafanyabiashara, akaamua kuacha mbuzi ale kulingana na urefu wa kamba yake. Huu ulikuwa ni mwanzo kwa serikali kushindwa kufahamu kiwango cha sukari kilichoko ndani ya nchi na pia kiwango kinachohitajika kwa mwaka. Anayefuata ni Gulam Dewji ambaye ni Baba yake na Mohammed Dewji (Mo Dewji). Huyu ni Mwenyekiti wa MeTL Group na Mnunuzi na mwagizaji mkuu wa sukari kama malighafi kwa ajili ya viwanda vyake na pia kuuza kwenye soko laTanzania Bara. Huyu pia alikuwa anapewa special/exclusive permit ya kuagiza sukari Wa mwisho ni Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo ambaye ni mmoja wa inner circle ya Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons). Kwenye inner circle ya Sir Andy Chande huwezi kumkosa Edward Lowassa, Rostam Aziz na Balozi Juma Mwapachu. Kwa ku-refresh your mind, Unaweza kupitia hii H

BREAKNEWZ MAKONDA AMSIMAMISHA KAZI AFISA UTUMISHI

Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda amemsimamisha kazi Afisa Utumishi wa Manispaa ya Ilala kwa kutowagundua watumishi hewa 11. Tarehe 2 Mei Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda aliwapa kiapo cha kazi wakuu wa Idara zote za jiji la Dar pamoja na maafisa Utumishi wa halmashauri za jiji wasaini kiapo cha kazi mbele ya Mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya baada ya kubainika kutoa taarifa zisizo za kweli dhidi ya kuwepo kwa watumishi hewa katika idara zao baada ya kubainika watumishi hewa wengine 209 katika Uchunguzi wa Siku chache zilizopita. Miongoni mwa masharti yaliokuwapo katika kiapo hicho ni kwamba iwapo ikigundulika kuwapo kwa watumishi hewa katika idara husika baada wiki moja, Afisa utumishi au mkuu wa idara hiyo atalipa gharama za mishahara iliyopotea, kushitakiwa kwa uhujumu uchumi, kuachishwa kazi lakini pia kufikishwa mahakamani. Hatua ya kusaini na kula kiapo inatokana na baadhi ya wakuu wa idara pamoja na maafisa Utumishi katika jiji la DSM kudaiwa kutoa taarifa za uongo kwa Mkuu wa mkoa Paul Makonda na wakuu wa wilaya za jiji hilo baada ya kutoa idadi ndogo ya watumishi hewa kwa mkoa wa dsm ambao walikuwa 74 tu, huku uhakiki wa sasa uliofanywa na tume maalum ukibaini watumishi hewa 209 ambao wametafuna kiasi cha takribani shilingi k

TRA YAGAWA SUKARI BURE LINDI

Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi. Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar. Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Milioni 246. Sukari hiyo imegawiwa kwa taasisi 31 mkoani humo baada ya TFDA kuthibitisha kuwa sukari iko salama kwa matumizi ya binadamu. Akizungumza wakati wa ugawaji wa sukari hiyo Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipakodi TRA Richard Kayombo amesema baada ya kukamatwa kwa bidhaa hizo TRA kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali ikiwemo ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi, iliamriwa sukari hiyo kuigawa kwa watu wenye uhitaji katika mkoa huo zikiwemo taasisi za elimu, Afya, kambi za wazee na Jeshi la magereza. Chanzo: TBC

kuhusu sukari mpya yaibuka tena

Na Mwandishi Wetu - JAMVI LA HABARI TAMKO la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini(TAKUKURU) kuwa Taasisi hiyo imeanza uchunguzi dhidi ya mfanyabiashara Haruni Daudi Zacharia limeibua mapya. Zacharia, ambaye ni mfanyabiashara maarufu na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa sukari hapa nchini na anayetuhumiwa kuficha bidhaa hiyo TAKUKURU imebaini kuwepo kwa njama za dhati za kutouza sukari iliyokutwa katika maghala hayo kulikofanywa na mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya Maghala ilipo sukari hiyo hapakuwa na dalili za upakiaji wa sukari hiyo ili iweze kusambazwa Katika eneo la Kitumbini kumekuwa na wananchi wengi wanaohitaji bidhaa hiyo na wachache sana waliweza kuuziwa licha ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo. Kumekuwepo na mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiasha huyo kwa kununua sukari yote toka viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko. Taarifa zaidi zinaeleza kufichuka kwa habari, ambayo kwa muda mrefu gazeti hili lilikuwa linaeleza namna mchezo unavyofanyika kwa mfanyabiashara huyo mwenye asili ya kiasia na mwenzake ambaye Salim Turk. Turk ni mbunge wa CCM katika jimbo la Mpendae Zanzibar. Turk anatajwa kuwa mbia mkubwa wa mfanyabiashara huyo, na anadaiwa kuwa amekuwa akitumia nafasi yake ya ubunge kujinufaisha kibiashara hasa katika sekta ya sukari kwa muda mrefu. Taarifa ambazo Jamvi La Habari imezipata zilieleza kuwa aliingiza tani 20000 kimagendo kutoka nje kwa kushirikiana na mfanyabiashara huyo, ambaye hivi sasa anachunguzwa na TAKUKURU kutokana na kitendo cha kuficha sukari. Wafanyabiashara hao , wamekuwa wakiidanganya serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Nchini(TRA) kwamba inaingiza sukari inayopitishwa kwenda nchi jirani na badala yake wanaiingiza nchini na kuendelea kuiuza sukari ambayo inaelezwa pia inaweza ikawa haina ubora. Licha ya Turky na Zacharia kuhusishwa katika suala la sukari, ambapo inaelezwa kuanzia mwaka 2009 mpaka 2012 pekee, zaidi ya Bilioni 462 zimepotea kwa udanganyifu wa wafanyabishara hao kwa kukwepa kodi. Vilevile taarifa zinasema, kwa miaka kadhaa sasa, serikali imekuwa ikipata hasara ya kukwepwa kodi kwa zaidi ya bilioni 300 kila mwaka kunakofanywa na wafanyabiashara hao Taarifa zaidi ilizozipata JAMVI LA HABARI, zinaeleza kuwa, uingizaji huo holela wa sukari nchini, unaenda sambamba na uamuzi wa serikali ya awamu ya nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete iliyoamua kutoa vibali kwa wafanyabiashara wachache nchini ili waruhusiwe kuagiza sukari kutoka nje, ambapo suala nzima la ugawaji wa vibali hivyo lilikuwa na utata mkubwa. Inaelezwa kuwa suala hili la ugawaji wa vibali vya sukari, liliondolewa katika Wizara ya Kilimo na Chakula na kupelekwa kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, ambayo ilikuwa inashughulika na ugawaji wa vibali hivyo. “Huu ni mchezo na taifa linakosa mapato mengi. Dalali wa vibali hivyo alikuwa mmoja wa mameya wa jiji la Dar es Salaam aliyekuwa anawapeleka wafanyabiashara mbalimbali kupata vibali vya kuagiza sukari nchi za nje,’’kilisema chanzo chetu cha habari.

Friday, May 6, 2016

Nafasi za kazi

Legal Internee Views 241 Apply Before: 13 May 2016 Company > Jurisolutions & Associates Location > Dar Es Salaam Position Type > Internship Organization Type > Company Position Description We have a vacancy for a legal internee with our law firm located downtown Dar es Salaam. The internee will be able to acquire knowledge and skills in the following areas: 1. Legal drafting 2. Interviewing clients 3. Court procedures 4. Filing documents in courts of law and tribunals 5. Preparing pleadings 6. Managing chamber diary 7. Managing files