Thursday, May 12, 2016

RAIS WA BRAZILI ATUMBULIWA JIPU

Mtu wangu kama utakuwa karibu na vyombo vya habari vya kimataifa story inayochukua headline sasa hivi ni kuhusu aliyekuwa Rais wa Brazil wa kwanza mwanamke Dilma Rousself kusimamishwa kazi ya urais. Hatua hiyo imekuja baada ya Bunge la Seneti Brazil kupiga kura kuidhinisha kutokuwa na imani na kiongozi huyo wa Taifa ambapo amesimamishwa kwa siku zisizozidi 180 wakati bunge hilo likichunguza tuhuma za rushwa zinazomkabili. Masenata 55 waliunga kuidhinishwa kura hiyo ya kutokuwa na iman na 22 walipinga.

No comments:

Post a Comment