Friday, May 6, 2016

Diddy aongoza orodha ya Forbes ya wana hip hop watano wenye mkwanja zaidi

Forbes wametoa orodha mpya ya wasanii wa hip hop wenye fedha zaidi, The Forbes Five. Diddy ameongoza orodha hiyo mwaka huu kwa kuwa na utajiri ufikao dola milioni 750. Nafasi ya pili imekamatwa na Dr Dre mwenye dola milioni 710 huku Jay Z akifuatia kwa dola milioni 610. Mwanzilishi wa Cash Money, Birdman amefuatia katika nafasi ya nne akiwa na dola milioni 110. Drake amechukua nafasi ya 50 Cent na kukamata nafasi ya tano kwa utajiri wa dola milioni 60.

No comments:

Post a Comment