Friday, May 6, 2016

Mrisho Mpoto kateuliwa kuwa balozi wa TACAIDS

Mgodi wa Dhahabu wa Geita Gold (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kupambana na Ukimwi nchini (TACAIDS) imemteua Staa wa kugani mashairi bongo Mrisho Mpoto kuwa balozi wa kampeni ya Kili Challenge. Kili Challenge ni Kampeni inayolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kutunisha mfuko wa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI. Mpoto ameteuliwa kuwakilisha na kuitangaza kampeni hii ili kusaidiana na serikali pamoja na wadau mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment