Friday, May 6, 2016

kesi ya aliyekuwa kamishina Wa tra Leo imefikia hapa

Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic tawi la Tanzania pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare wamefika Mahakama kuu leo May 06 2016 ili kusikiliza rufaa ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha. Rufani hiyo imesikilizwa leo ambapo mahakama kuu imefuta pingamizi hilo kutokana na kuwa na dosari hivyo shauri linarudi kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuendelea pale lilipokuwa limeishia na upande wa Jamhuri wanaweza kuandaa tena rufani na kufungua tena.

No comments:

Post a Comment