Friday, May 6, 2016

Neymar hajatajwa kwenye kikosi cha Brazil kitakacho shiriki copa america

Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Dunga tayari ameshatangaza kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Copa America kwa mwaka 2016, likiwa jina la Neymar halipo katika list hiyo ya majina 23, Neymar anakosekana katika list hiyo kutokana na FC Barcelona kuomba asiitwe staa huyo kwa ajili ya michuano hiyo. Neymar kaachwa katika kikosi kitachoshiriki michuano hiyo maalum kwa ajili ya kuadhimisha miaka 100 ya Copa America kutokana na FC Barcelona kumuomba Dunga amuache Neymar, kwani hawezi kucheza michuano miwili ndani ya kipindi kimoja cha majira ya joto kwa sababu atapata uchovu ila atajumuishwa katika kikosi kitakachoshiriki michuano ya Olympic. List ya wachezaji wa Brazil walioitwa kwa ajili ya michuano maalum ya Copa America 2016 Magoikipa: Alisson (Internacional), Diego Alves (Valencia) and Ederson (Benfica), Mabeki: Daniel Alves (Barcelona), Fabinho (Monaco), Filipe Luis (Atletico Madrid), Douglas Santos (Atletico Mineiro), Miranda (Inter Milan), Gil (Shandong Luneng), Marquinhos (Paris Saint-Germain), Rodrigo Caio (Sao Paulo) Viungo: Luiz Gustavo (Wolfsburg), Elias (Corinthians), Casemiro (Real Madrid), Rafinha (Barcelona), Renato Augusto (Beijing Guoan), Philippe Coutinho (Liverpool), Lucas Lima (Santos) na Willian (Chelsea). Washambuliaji: Douglas Costa (Bayern Munich), Hulk (Zenit), Ricardo Oliveira (Santos) na Gabriel (Santos)

No comments:

Post a Comment