Friday, May 6, 2016

TRA Yazidi Kuvuka Malengo Ya Ukusanyaji Mapato ....Yakusanya Trioni 1.035 Mwezi Uliopita Sawa na Asilimia 99.5

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) kwa mwezi uliopita imekusanya Sh.Trioni 1.035 ambayo ni sawa na asilimia 99.5 ya lengo kukusanya sh.trioni 1.040 . Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa katika makusanyo ya miezi 10 wameweza kukusanya sh. Trioni 10.92 ambayo sawa na asilimia 99 ya lengo ya sh.trioni 11.02 katika lengo la kipindi hicho. Amesema kuwa TRA imedhamiria kukusanya zaidi ya sh. Trioni 1.4 na kuvuka lengo la mwaka wa fedha wa 2015/2016 katika miezi miwili ya kumaliza mwaka wa fedha ambalo ni sh. Trioni 12.3. Kidata amesema kuwa TRA itaendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha inafikia lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2015 / 2016 licha kuwepo kwa changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo. Amesema kuwa wananchi wamejua umuhimu wa kodi na kuanza kutoa ushirikiano katika kudhibiti mianya ya magaendo, pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ikiwa katika usimamizi wa mifumo ya mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu wowote.

No comments:

Post a Comment