Friday, May 6, 2016

SERIKALI YAWATEGEA WAFANYABIASHARA MAENEO

Dar es Salaam. Zaidi ya wafanyabiashara wadogo 2000 waliokuwa wakifanya shughuli zao maeneo yasiyo rasmi katika Manispaa ya Ilala, wametengewa masoko manne kwa ajili ya kufanya biashara zao. Masoko hayo ni Kigogo Fresh, lililopo maeneo ya Pugu, soko la Ukonga karibu na Gereza la Ukonga, Tabata Muslim na Soko la Kivule, ambayo wafanyabiashara hao maarufu kama ‘wamachinga’ wanatakiwa kwenda. Wafanyabiashara waliolengwa zaidi ni wale ambao wanafanya shughuli zao kwa kupanga barabarani hususan barabara ya mabasi ya mwendo kasi na katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo na Mnazi Mmoja kwenye manispaa hiyo. Hata hivyo, baadhi ya wafanyabishara hao wakizungumza na Mwananchi wameonyesha wasiwasi wao juu ya uamuzi huo wa kuwahamisha na kusema masoko hayo watakayoenda siyo rafiki kwao na biashara wanazozifanya. Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi amesema jana kuwa utaratibu wa kuwapangia maeneo wafanyabiashara hao ulichelewa kwa sababu walikuwa katika mchakato wa kuwatambua ili mpango wao kuwapeleka maeneo hayo uende kwa ufanisi. “Mchakato wa kuwatambua umemalizika na leo, tumewaagiza viongozi waende kwenye ofisi ofisa wa mipango miji kwa ajili ya kupewa utaratibu wa jinsi mtawanyo wa wafanyabiashara hao,” amesema Mgurumi. Ameongeza kuwa mazingira ya masoko hayo manne yapo vizuri na yana uwezo wa kubeba wafanyabiashara zaidi ya 2000, kwani makadirio ya manispaa ni wafanyabiashara 6000 katika masoko hayo. Kwa mujibu wa Mngulumi, Mei 9 mwaka huu, manispaa ikishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama itaanza operesheni ya kuwaondoa kinguvu maeneo hayo na kuwataka wafanyabiashara hao kutumia siku zilizobaki kuwasiliana na viongozi wao kujua utaratibu wa kuondoka. “Hapa leo ni kama nakazia tu uamuzi huu ila tulishawatangazia hapo awali.Kwa hiyo sitarajia kuona watu maeneo hayo ikifika Mei 9, ukibainika utakamatwa na utalipa faini au kupelekwa mahakamani,” “Operesheni hii pia itaenda sambamba na kuwaondoa wenye gereji bubu na wale wote wanaosha magari maeneo yasiyo rasmi,” amesema Mgurumi. Mohamed Twaha ambaye anafanya shughuli zake za kupanga bidhaa pembezoni mwa barabara ya mwendo kasi Kariakoo amesema kuwahamisha na kuwapeleka katika masoko hayo njia mbadala badala yake manispaa itengee mitaa maalumu kwa ajili ya kufanya biashara zao. “Hatupingi kuondoka maeneo haya. Lakini huko tunakopelekwa ni majanga, Rais John Magufuli anasisitiza watu wafanye kazi na sisi tumejitoa ila huko tukoenda hatuwezi kufanya kazi,” amesema Twaha. Kwa upande Tambwe Muhidini anayefanya shughuli zake Mnazi Mmoja amesema wanapenda kufanya biashara katika maeneo hayo kwa sababu kuna wingi wa watu na wateja wao wakubwa watokea katika ofisi mbalimbali zilizopo katikati ya jiji. “Hatuchafui jiji, fedha za usafi tunatoa kila siku. Kwa nini Serikali inatufanyia hivi tunaiomba ifikirie mara mbili la sivyo wafanyabiashara wa maeneo hayo

No comments:

Post a Comment