Pata habari motomoto za kitaifa na kimataifa za kisiasa,michezo,burudani,vibwenga vya masta wa bongo na nje ,breaknewz ,kilimo cha kisasa,na nyingine nyingi
Thursday, May 12, 2016
RAIS WA BRAZILI ATUMBULIWA JIPU
Mtu wangu kama utakuwa karibu na vyombo vya habari vya kimataifa story inayochukua headline sasa hivi ni kuhusu aliyekuwa Rais wa Brazil wa kwanza mwanamke Dilma Rousself kusimamishwa kazi ya urais.
Hatua hiyo imekuja baada ya Bunge la Seneti Brazil kupiga kura kuidhinisha kutokuwa na imani na kiongozi huyo wa Taifa ambapo amesimamishwa kwa siku zisizozidi 180 wakati bunge hilo likichunguza tuhuma za rushwa zinazomkabili.
Masenata 55 waliunga kuidhinishwa kura hiyo ya kutokuwa na iman na 22 walipinga.
MTOTO Wa CHACHA WANGWE AFIKISHWA MAHAKAMANI
BOB Chacha Wangwe (24), mtoto wa mwanasiasa marehemu Chacha Wangwe, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii anaandika Faki Sosi.Akisoma kesi hiyo namba 167, Paul Kagoshi mbele ya Waliarandwe Rema, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo amesema kuwa, Bob Chacha Wangwe amefikishwa mahakamani hapo kwa kutenda kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake Facebook.Mshitakiwa anadaiwa kutenda hayo tarehe 15 Machi na kwamba alichapicha maneno haya Tanzania ni ambayo….inajaza chuki wananchi … matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania bara kwa sababu za kijinga.Mtuhumiwa amekiri kutenda makosa hayo hivyo amerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 17 Mei mwaka huu.
Monday, May 9, 2016
Wajue wafanya biashara wakubwa Wa sukari tanzania
mstakabali wa sukari na hatima ya viwanda vya sukari nchini.
Sukari yote nchini inayoagizwa kutoka nje kwa kiasi kikubwa ilikuwa inaagizwa na hawa matajiri wakubwa nchini kama wanavyoonekana kwenye picha.
Hawa ni baadhi ya matajiri ambao wanamiliki soko la sukari nchini ambalo wakati wa utawala wa Rais Kikwete, hakuweza kuwadhibiti ili kuvilinda viwanda vya sukari nchini na afya za walaji.
Hawa kwenye picha hapo chini ni aina ya watu wanaoitwa sugar industries movers and shakers katika jumuiya ya wafanyabiashara nchini.
Kutoka kushoto ni Harun Daudi Zakaria ambaye juzi vikosi vya usalama nchini vilikuta kwenye magodauni yake huko Mbagala na Tabata tani zaidi ya 4,600 ambazo inasemakana zilikuwa zimefichwa, kwa lugha ya kisheria wanasema hoarding commodities. Huyu wakati mwingine alikuwa anapewa vibali ambavyo waingereza wanasema special/exclusive permit kununua au kuagiza sukari kwa ajili ya soko la Zanzibar.
Anayefuatia ni Said Salim Bakhresa ambaye hununua sukari nchini au kuagiza nje ya nchi maelfu ya tani za sukari kama malighafi kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa kwenye viwanda vyake.
Anayefuatia ni Reginald Mengi ambaye ana viwanda vya vinywaji. Hununua sukari nchini au kuagiza nje ya nchi maelfu ya tani kama malighafi kwa ajili ya viwanda vyake mbali mbali.
Anayefuata ni Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ambaye baada ya kushindwa vita ya sukari kutokana na nguvu kubwa waliyonayo hawa wafanyabiashara, akaamua kuacha mbuzi ale kulingana na urefu wa kamba yake. Huu ulikuwa ni mwanzo kwa serikali kushindwa kufahamu kiwango cha sukari kilichoko ndani ya nchi na pia kiwango kinachohitajika kwa mwaka.
Anayefuata ni Gulam Dewji ambaye ni Baba yake na Mohammed Dewji (Mo Dewji). Huyu ni Mwenyekiti wa MeTL Group na Mnunuzi na mwagizaji mkuu wa sukari kama malighafi kwa ajili ya viwanda vyake na pia kuuza kwenye soko laTanzania Bara. Huyu pia alikuwa anapewa special/exclusive permit ya kuagiza sukari
Wa mwisho ni Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo ambaye ni mmoja wa inner circle ya Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons). Kwenye inner circle ya Sir Andy Chande huwezi kumkosa Edward Lowassa, Rostam Aziz na Balozi Juma Mwapachu.
Kwa ku-refresh your mind, Unaweza kupitia hii H
BREAKNEWZ MAKONDA AMSIMAMISHA KAZI AFISA UTUMISHI
Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda amemsimamisha kazi Afisa Utumishi wa Manispaa ya Ilala kwa kutowagundua watumishi hewa 11.
Tarehe 2 Mei Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda aliwapa kiapo cha kazi wakuu wa Idara zote za jiji la Dar pamoja na maafisa Utumishi wa halmashauri za jiji wasaini kiapo cha kazi mbele ya Mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya baada ya kubainika kutoa taarifa zisizo za kweli dhidi ya kuwepo kwa watumishi hewa katika idara zao baada ya kubainika watumishi hewa wengine 209 katika Uchunguzi wa Siku chache zilizopita.
Miongoni mwa masharti yaliokuwapo katika kiapo hicho ni kwamba iwapo ikigundulika kuwapo kwa watumishi hewa katika idara husika baada wiki moja, Afisa utumishi au mkuu wa idara hiyo atalipa gharama za mishahara iliyopotea, kushitakiwa kwa uhujumu uchumi, kuachishwa kazi lakini pia kufikishwa mahakamani.
Hatua ya kusaini na kula kiapo inatokana na baadhi ya wakuu wa idara pamoja na maafisa Utumishi katika jiji la DSM kudaiwa kutoa taarifa za uongo kwa Mkuu wa mkoa Paul Makonda na wakuu wa wilaya za jiji hilo baada ya kutoa idadi ndogo ya watumishi hewa kwa mkoa wa dsm ambao walikuwa 74 tu, huku uhakiki wa sasa uliofanywa na tume maalum ukibaini watumishi hewa 209 ambao wametafuna kiasi cha takribani shilingi k
TRA YAGAWA SUKARI BURE LINDI
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi.
Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar.
Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Milioni 246.
Sukari hiyo imegawiwa kwa taasisi 31 mkoani humo baada ya TFDA kuthibitisha kuwa sukari iko salama kwa matumizi ya binadamu.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa sukari hiyo Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipakodi TRA Richard Kayombo amesema baada ya kukamatwa kwa bidhaa hizo TRA kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali ikiwemo ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi, iliamriwa sukari hiyo kuigawa kwa watu wenye uhitaji katika mkoa huo zikiwemo taasisi za elimu, Afya, kambi za wazee na Jeshi la magereza.
Chanzo: TBC
kuhusu sukari mpya yaibuka tena
Na Mwandishi Wetu - JAMVI LA HABARI
TAMKO la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini(TAKUKURU) kuwa Taasisi hiyo imeanza uchunguzi dhidi ya mfanyabiashara Haruni Daudi Zacharia limeibua mapya.
Zacharia, ambaye ni mfanyabiashara maarufu na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa sukari hapa nchini na anayetuhumiwa kuficha bidhaa hiyo
TAKUKURU imebaini kuwepo kwa njama za dhati za kutouza sukari iliyokutwa katika maghala hayo kulikofanywa na mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya Maghala ilipo sukari hiyo hapakuwa na dalili za upakiaji wa sukari hiyo ili iweze kusambazwa
Katika eneo la Kitumbini kumekuwa na wananchi wengi wanaohitaji bidhaa hiyo na wachache sana waliweza kuuziwa licha ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo.
Kumekuwepo na mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiasha huyo kwa kununua sukari yote toka viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko.
Taarifa zaidi zinaeleza kufichuka kwa habari, ambayo kwa muda mrefu gazeti hili lilikuwa linaeleza namna mchezo unavyofanyika kwa mfanyabiashara huyo mwenye asili ya kiasia na mwenzake ambaye Salim Turk. Turk ni mbunge wa CCM katika jimbo la Mpendae Zanzibar.
Turk anatajwa kuwa mbia mkubwa wa mfanyabiashara huyo, na anadaiwa kuwa amekuwa akitumia nafasi yake ya ubunge kujinufaisha kibiashara hasa katika sekta ya sukari kwa muda mrefu.
Taarifa ambazo Jamvi La Habari imezipata zilieleza kuwa aliingiza tani 20000 kimagendo kutoka nje kwa kushirikiana na mfanyabiashara huyo, ambaye hivi sasa anachunguzwa na TAKUKURU kutokana na kitendo cha kuficha sukari.
Wafanyabiashara hao , wamekuwa wakiidanganya serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Nchini(TRA) kwamba inaingiza sukari inayopitishwa kwenda nchi jirani na badala yake wanaiingiza nchini na kuendelea kuiuza sukari ambayo inaelezwa pia inaweza ikawa haina ubora.
Licha ya Turky na Zacharia kuhusishwa katika suala la sukari, ambapo inaelezwa kuanzia mwaka 2009 mpaka 2012 pekee, zaidi ya Bilioni 462 zimepotea kwa udanganyifu wa wafanyabishara hao kwa kukwepa kodi.
Vilevile taarifa zinasema, kwa miaka kadhaa sasa, serikali imekuwa ikipata hasara ya kukwepwa kodi kwa zaidi ya bilioni 300 kila mwaka kunakofanywa na wafanyabiashara hao
Taarifa zaidi ilizozipata JAMVI LA HABARI, zinaeleza kuwa, uingizaji huo holela wa sukari nchini, unaenda sambamba na uamuzi wa serikali ya awamu ya nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete iliyoamua kutoa vibali kwa wafanyabiashara wachache nchini ili waruhusiwe kuagiza sukari kutoka nje, ambapo suala nzima la ugawaji wa vibali hivyo lilikuwa na utata mkubwa.
Inaelezwa kuwa suala hili la ugawaji wa vibali vya sukari, liliondolewa katika Wizara ya Kilimo na Chakula na kupelekwa kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, ambayo ilikuwa inashughulika na ugawaji wa vibali hivyo.
“Huu ni mchezo na taifa linakosa mapato mengi. Dalali wa vibali hivyo alikuwa mmoja wa mameya wa jiji la Dar es Salaam aliyekuwa anawapeleka wafanyabiashara mbalimbali kupata vibali vya kuagiza sukari nchi za nje,’’kilisema chanzo chetu cha habari.
Friday, May 6, 2016
Nafasi za kazi
Legal Internee
Views 241
Apply Before: 13 May 2016
Company > Jurisolutions & Associates
Location > Dar Es Salaam
Position Type > Internship
Organization Type > Company
Position Description
We have a vacancy for a legal internee with our law firm located downtown Dar es Salaam. The internee will be able to acquire knowledge and skills in the following areas: 1. Legal drafting 2. Interviewing clients 3. Court procedures 4. Filing documents in courts of law and tribunals 5. Preparing pleadings 6. Managing chamber diary 7. Managing files
SERIKALI YAWATEGEA WAFANYABIASHARA MAENEO
Dar es Salaam. Zaidi ya wafanyabiashara wadogo 2000 waliokuwa wakifanya shughuli zao maeneo yasiyo rasmi katika Manispaa ya Ilala, wametengewa masoko manne kwa ajili ya kufanya biashara zao.
Masoko hayo ni Kigogo Fresh, lililopo maeneo ya Pugu, soko la Ukonga karibu na Gereza la Ukonga, Tabata Muslim na Soko la Kivule, ambayo wafanyabiashara hao maarufu kama ‘wamachinga’ wanatakiwa kwenda.
Wafanyabiashara waliolengwa zaidi ni wale ambao wanafanya shughuli zao kwa kupanga barabarani hususan barabara ya mabasi ya mwendo kasi na katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo na Mnazi Mmoja kwenye manispaa hiyo.
Hata hivyo, baadhi ya wafanyabishara hao wakizungumza na Mwananchi wameonyesha wasiwasi wao juu ya uamuzi huo wa kuwahamisha na kusema masoko hayo watakayoenda siyo rafiki kwao na biashara wanazozifanya.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi amesema jana kuwa utaratibu wa kuwapangia maeneo wafanyabiashara hao ulichelewa kwa sababu walikuwa katika mchakato wa kuwatambua ili mpango wao kuwapeleka maeneo hayo uende kwa ufanisi.
“Mchakato wa kuwatambua umemalizika na leo, tumewaagiza viongozi waende kwenye ofisi ofisa wa mipango miji kwa ajili ya kupewa utaratibu wa jinsi mtawanyo wa wafanyabiashara hao,” amesema Mgurumi.
Ameongeza kuwa mazingira ya masoko hayo manne yapo vizuri na yana uwezo wa kubeba wafanyabiashara zaidi ya 2000, kwani makadirio ya manispaa ni wafanyabiashara 6000 katika masoko hayo.
Kwa mujibu wa Mngulumi, Mei 9 mwaka huu, manispaa ikishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama itaanza operesheni ya kuwaondoa kinguvu maeneo hayo na kuwataka wafanyabiashara hao kutumia siku zilizobaki kuwasiliana na viongozi wao kujua utaratibu wa kuondoka.
“Hapa leo ni kama nakazia tu uamuzi huu ila tulishawatangazia hapo awali.Kwa hiyo sitarajia kuona watu maeneo hayo ikifika Mei 9, ukibainika utakamatwa na utalipa faini au kupelekwa mahakamani,”
“Operesheni hii pia itaenda sambamba na kuwaondoa wenye gereji bubu na wale wote wanaosha magari maeneo yasiyo rasmi,” amesema Mgurumi.
Mohamed Twaha ambaye anafanya shughuli zake za kupanga bidhaa pembezoni mwa barabara ya mwendo kasi Kariakoo amesema kuwahamisha na kuwapeleka katika masoko hayo njia mbadala badala yake manispaa itengee mitaa maalumu kwa ajili ya kufanya biashara zao.
“Hatupingi kuondoka maeneo haya. Lakini huko tunakopelekwa ni majanga, Rais John Magufuli anasisitiza watu wafanye kazi na sisi tumejitoa ila huko tukoenda hatuwezi kufanya kazi,” amesema Twaha.
Kwa upande Tambwe Muhidini anayefanya shughuli zake Mnazi Mmoja amesema wanapenda kufanya biashara katika maeneo hayo kwa sababu kuna wingi wa watu na wateja wao wakubwa watokea katika ofisi mbalimbali zilizopo katikati ya jiji.
“Hatuchafui jiji, fedha za usafi tunatoa kila siku. Kwa nini Serikali inatufanyia hivi tunaiomba ifikirie mara mbili la sivyo wafanyabiashara wa maeneo hayo
Diddy aongoza orodha ya Forbes ya wana hip hop watano wenye mkwanja zaidi
Forbes wametoa orodha mpya ya wasanii wa hip hop wenye fedha zaidi, The Forbes Five.
Diddy ameongoza orodha hiyo mwaka huu kwa kuwa na utajiri ufikao dola milioni 750. Nafasi ya pili imekamatwa na Dr Dre mwenye dola milioni 710 huku Jay Z akifuatia kwa dola milioni 610.
Mwanzilishi wa Cash Money, Birdman amefuatia katika nafasi ya nne akiwa na dola milioni 110. Drake amechukua nafasi ya 50 Cent na kukamata nafasi ya tano kwa utajiri wa dola milioni 60.
Mwanadada wa Kitanzania akamatwa China na madawa ya kulevya
image.jpeg
Mwanamke mmoja wa Kitanzania amekamatwa huko Guangzhou-China na kete kadhaa za madawa ya kulevya.
Bado jina lake halijafahamika.
Inasemekana anatokea Sinza-Dsm, kwa yoyote mwenye kuujua ukweli wa mahali anapoishi na ndugu zake anaweza kuwapa taarifa kuwa "shost" hali si nzuri huko kwa kina Mao Tse Tung.
Taatifa zaidi zinakujia...
SHERIKALI YAKAMATA SUKARI ILIYOFICHWA MBAGALA
Baada ya muda mfupi wa rais kusema kuwa kuna wafanyabiashara wameficha Sukari, muda huu imeripotiwa kuwa huko Mbagala kuna Sukari ya zaidi ya tani 4,900 kwenye ghala la mfanya biashara mmoja na imeelezwa zitachukuliwa hatua stahiki.
chanzo; TBC, habari mpasuko
RAIS MAGUFULI AMESEMA WATAGAWA SUKARI BURE
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya walioficha Sukari na kutishia Kuichukua Sukari hiyo na Kuigawa Bure Kwa Wananchi. Rais Magufuli ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara walioficha sukari ili baadae waiuze kwa bei ya juu.
Amesema wafanyabiashara hao wenye tamaa ya pesa walikuwa wakifuata sukari iliyo Expire huko Brazili na kuileta nchini ili watengeneze faida na ndo maana serikali iliwapiga marufuku kuagiza.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akiwasalimia wananchi wa Katesh, Mkoani Manyara. Rais ametoka Mkoani Dodoma leo, anaelekea Mkoani Arusha kwa usafiri wa gari.
Akiongea na mamia ya wananchi hao waliojitokeza kumlaki njiani, Rais Magufuli amewatoa hofu wananchi kuhusu uhaba wa sukari kwa kuwa tayari wako katika mchakato wa kuagiza makontena ya sukari nje ya nchi ili kuwakabili wafanyabiashara walioficha bidhaa hiyo.
Amesema kwa taarifa alizonazo, kuna mfanyabiashara alienda akanunua sukari pale Kilombero zaidi ya tani 3000 na hataki kuzichukua hadi leo
Pia amesema kuna mwingine ana godauni huko Mbagala yenye tani 4000 ambazo hataki kuzitoa ili wananchi wakose sukari.
Rais Magufuli amesema ameviagiza vyombo vya dola viwafuatilie ili ikithibitika sukari waliificha basi ichukuliwe na kugawiwa bure kwa wananchi na pia watapigwa marufuku kufanya biashara yoyote hapa nchini.
HIZI HAPA PICHA ZA GARI YA HARMONIZER
Baada ya show zake ambazo hazifiki hata 15 toka ametusua kupitia single yake ya Aiyola mkali huyu kutoka WCB ameonyesha bidii ikiwekwa popote kuna matunda.
Ni gari aina ya Mark X ambapo Mmiliki wa label ya WCB, Diamond Platnumz alimpongeza na kuandika…’Kama nikusiivyo siku zote ni juhudi na Nidhamu yako ndio itayokufanya upate matunda ya kazi yako….. Usiache unyenyekevu, kuheshimu mkubwa na Mdogo, Kumuomba na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila hatua ndogo Uipigayo…. Congrats kwa your New Ride’ – Diamond
Hizi ni picha 10 za muonekano wa gari hiyo mpya ya Harmonize kutoka WCB
HII HAPA HABARI KUHUSU LOWASA
Ukimya wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa UKAWA,Edward Lowassa umezua mjadala kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya CCM.Kikao cha Kamati Kuu kimefanyika jana hapa Dodoma.
Mjadala ulianza pale Mwenyekiti Kikwete alipochagiza maelezo yake ya chama kuendelea kufanya maandalizi ya chaguzi zijazo na kutobweteka. Mwenyekiti alisema kuwa Lowassa bado ana uungwaji mkono na nguvu ya kisiasa na hutumia ukimya kujijenga zaidi.
Mwenyekiti alionya kuwa Lowassa hakufika mwisho na chama chapaswa kuutazama ukimya wake wa kuchangia na kutoa hoja juu ya Serikali ya Rais Magufuli kwa jicho la tatu. Wajumbe wote wa KK walikubaliana na Mwenyekiti Kikwete.
Wakati huohuo,Rais Magufuli ameaswa kuwa 'mpole kiasi' atakapoukwaa uenyekiti wa taifa wa CCM mnamo mwezi Juni mwaka huu. Imesemwa kuwa wanachama wa chama cha siasa hutendewa mambo kwa upole ili wabaki chamani na kukijenga chama. KK imeunga mkono hatua za Rais na Serikali yake kutumbua majipu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
SIMBA KUSHUSHWA DARAJA KWA KUKIUKA AGIZO LA FIFA
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limeipiga faini ya Franc 2,000 za Uswisi (Sh 4,582,000 za Tanzania), Klabu ya Simba baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupuuza maagizo ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Chamber) ya FIFA.
Kamati ya idara hiyo iliyokutana na Aprili 20, 2016 huko Zurich, Uswis ilitumia Franc 500 (sawa na Sh 1,145,500) hivyo Simba pia imeagizwa kuzilipa ikiwa ni gharama za kikao cha kufuatilia utekelezaji sakata la mchezaji huyo, raia wa Kenya.
Simba imeelezwa kupuuza kumlipa mchezaji Donald Musoti Omanua kwa wakati tangu mkataba wake uvunjwe.
Musoto aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa alilalamika FIFA ambayo iliona ana hoja na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola 29,250 (sawa na Sh 62.8 milioni) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni.
Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.
Felix Majani, Mwanasheria wa Musoti, ambaye pia ni mmoja wa wanasheria wa FIFA, alifungua kesi katika shirikisho hilo kuwashitaki Simba kwa kukiuka makubaliano ya mkataba na mteja wake.
Kwa kosa hilo Simba inatakiwa kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016. TFF imekuwa nakala na maagizo kuisimamia Simba inalipa kiasi hicho cha fedha.
Simba imeagizwa kulipa stahiki zote za Mosoti ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016.
Katika barua hiyo ambayo TFF ina nakala yake, Simba imepewa amri ya kuhakikisha inalipa na isipotekeleza agizo hilo mara moja itakatwa pointi tatu katika mechi zake Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara –VPL.
FIFA imekwenda mbali zaidi ikisema ikiwa klabu hiyo kama haitalipa katika muda uliopangwa yaani siku 30 kutoka sasa, FIFA itaishusha Simba daraja kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara hadi Ligi Daraja la Kwanza au zaidi.
Kwa upande wake, TFF imagizwa kuhakikisha uamuzi huo unasimamiwa vema utekelezwaji wa maagizo hayo vinginevyo itachukuliwa hatua stahiki ikiwamo kuiondoa Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
mkurungezi arudi nyumbani kwake kwa miguu leo
Mheshimiwa DED amerejea nyumbani kwake kwa miguu baada ya kusimamwishwa kazi na Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa kudaiwa kulipa mishahara hewa kwa watumishi nane na kusbabishia Serikali hasara.... hapa kazi tu
TRA Yazidi Kuvuka Malengo Ya Ukusanyaji Mapato ....Yakusanya Trioni 1.035 Mwezi Uliopita Sawa na Asilimia 99.5
MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) kwa mwezi uliopita imekusanya Sh.Trioni 1.035 ambayo ni sawa na asilimia 99.5 ya lengo kukusanya sh.trioni 1.040 .
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa katika makusanyo ya miezi 10 wameweza kukusanya sh. Trioni 10.92 ambayo sawa na asilimia 99 ya lengo ya sh.trioni 11.02 katika lengo la kipindi hicho.
Amesema kuwa TRA imedhamiria kukusanya zaidi ya sh. Trioni 1.4 na kuvuka lengo la mwaka wa fedha wa 2015/2016 katika miezi miwili ya kumaliza mwaka wa fedha ambalo ni sh. Trioni 12.3.
Kidata amesema kuwa TRA itaendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha inafikia lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2015 / 2016 licha kuwepo kwa changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo.
Amesema kuwa wananchi wamejua umuhimu wa kodi na kuanza kutoa ushirikiano katika kudhibiti mianya ya magaendo, pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ikiwa katika usimamizi wa mifumo ya mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu wowote.
Mrisho Mpoto kateuliwa kuwa balozi wa TACAIDS
Mgodi wa Dhahabu wa Geita Gold (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kupambana na Ukimwi nchini (TACAIDS) imemteua Staa wa kugani mashairi bongo Mrisho Mpoto kuwa balozi wa kampeni ya Kili Challenge.
Kili Challenge ni Kampeni inayolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kutunisha mfuko wa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI. Mpoto ameteuliwa kuwakilisha na kuitangaza kampeni hii ili kusaidiana na serikali pamoja na wadau mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Jengo La NSSF La Eneo La Akiba Lawaka Moto
Jengo lililoko eneo la akiba posta jijini Dar es salaam limeripotiwa kuwaka moto kuanzia majira ya jioni na chanzo cha moto huo kinasemekana ni mtungi wa gesi kulipuka na kusababisha moto.
Inasemekana hakuna madhara makubwa kutokana na zimamoto kufika kwa wakati katika eneo la tukio.
Tibaijuaka :wataisoma namba
Dodoma. Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka jana alikuwa mkali bungeni akisema yeye si mwizi na kuwabeza wanaomuita hivyo kuwa wataisoma namba.
Profesa Tibaijuka alifikia hatua hiyo baada ya kuhamaki kutokana na baadhi ya wabunge wa upinzani kupaza sauti na kumuita mwizi wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria.
Profesa Tibaijuka alianza kwa kuwataka wabunge wamuunge mkono Rais John Magufuli kwa kuwa amechaguliwa na wananchi.
“Wenzetu ambao kazi yao ni kuja kutusimamia sisi (upinzani) wana haki ya kusema wanayoyasema, lakini hata sisi tuna haki ya kuyaweka vizuri ili yaeleweke kwa wananchi,” alisema.
Profesa Tibaijuka alisema upinzani ukifilisika utabaki kukemea kwa sababu ni lazima tu useme kitu, Bunge linageuka kijiwe na bungeni si mahali pa kupeleka hoja za vijiweni.
Kauli hiyo iliwakera wabunge wa upinzani ambao walianza kupaza sauti zao dhidi yake, hali iliyoonekana kumchanganya.
Akirejea hotuba ya msemaji wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu kuwa Tanganyika inainyonya Zanzibar na kuifanya koloni lake, Profesa Tibaijuka alihoji: “Tanganyika inainyonya Zanzibar katika lipi? Hili ni jambo la kujiuliza. Nimejiuliza mimi kama mchumi. Kazi yangu ya kwanza nyinyi mnanijua nilikuwa kwenye shirika la makazi duniani, hamjui kwamba nilikuwa kwenye Shirika la Biashara la Dunia?” alihoji.
Kutokana na zomeazomea kuendelea, Spika wa Bunge, Job Ndugai aliingilia kati: “Waheshimiwa wabunge namlinda mzungumzaji, naomba muwe wavumilivu. Mheshimiwa Profesa endelea.
“Kwa wale wanaosema nimeiba mtaisoma namba, mimi si mtu wa kutishwa na vitu vya ovyoovyo. Mimi sitishwi na hoja za ovyoovyo, huyo (mtu) akaisome namba. Nasimama hapa kwa sababu nataka nitetee vitu. Mtu anapopotosha anaweza kuleta hatari. Tanganyika kwa mtizamo wa kiuchumi haiwezi kuinyonya Zanzibar.
“Katika Dunia ya ustaarabu unasikia hoja. Lissu hapa angeweza kuzomewa, lakini wastaarabu wakamsikiliza wamekomaa kisiasa,” alisema huku baadhi ya wabunge wakiendelea kumzomea.
Tibaijuka aliwahi kuwa waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete na aliondolewa baada ya kutuhumiwa kupata mgawo wa fedha za Tegeta Escrow.
Neymar hajatajwa kwenye kikosi cha Brazil kitakacho shiriki copa america
Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Dunga tayari ameshatangaza kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Copa America kwa mwaka 2016, likiwa jina la Neymar halipo katika list hiyo ya majina 23, Neymar anakosekana katika list hiyo kutokana na FC Barcelona kuomba asiitwe staa huyo kwa ajili ya michuano hiyo.
Neymar kaachwa katika kikosi kitachoshiriki michuano hiyo maalum kwa ajili ya kuadhimisha miaka 100 ya Copa America kutokana na FC Barcelona kumuomba Dunga amuache Neymar, kwani hawezi kucheza michuano miwili ndani ya kipindi kimoja cha majira ya joto kwa sababu atapata uchovu ila atajumuishwa katika kikosi kitakachoshiriki michuano ya Olympic.
List ya wachezaji wa Brazil walioitwa kwa ajili ya michuano maalum ya Copa America 2016
Magoikipa: Alisson (Internacional), Diego Alves (Valencia) and Ederson (Benfica), Mabeki: Daniel Alves (Barcelona), Fabinho (Monaco), Filipe Luis (Atletico Madrid), Douglas Santos (Atletico Mineiro), Miranda (Inter Milan), Gil (Shandong Luneng), Marquinhos (Paris Saint-Germain), Rodrigo Caio (Sao Paulo)
Viungo: Luiz Gustavo (Wolfsburg), Elias (Corinthians), Casemiro (Real Madrid), Rafinha (Barcelona), Renato Augusto (Beijing Guoan), Philippe Coutinho (Liverpool), Lucas Lima (Santos) na Willian (Chelsea). Washambuliaji: Douglas Costa (Bayern Munich), Hulk (Zenit), Ricardo Oliveira (Santos) na Gabriel (Santos)
kesi ya aliyekuwa kamishina Wa tra Leo imefikia hapa
Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic tawi la Tanzania pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare wamefika Mahakama kuu leo May 06 2016 ili kusikiliza rufaa ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha.
Rufani hiyo imesikilizwa leo ambapo mahakama kuu imefuta pingamizi hilo kutokana na kuwa na dosari hivyo shauri linarudi kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuendelea pale lilipokuwa limeishia na upande wa Jamhuri wanaweza kuandaa tena rufani na kufungua tena.
UKAWA WATOKA NJE YA BUNGE LEO
UKAWA wametoka nje ya ukumbi wa Bunge Dodoma baada ya jana Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga kusema kuwa ‘Wabunge wote wa viti maalum CHADEMA ili wapate nafasi hizo ni lazima waitwe kwanza Baby‘
Kauli iliyopingwa na baadhi ya wabunge na kumtaka Naibu Spika kutumia kiti chake ili Mlinga atengue kauli yake, Mlinga alikubali kuitengua lakini Leo Mei 06 2106 hoja hiyo ikarejeshwa tena bungeni kuwa ni kauli ya udhalilishaji kwa wanawake.
Dr migiro ala kiapo leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.Hafla ya kuapishwa kwa Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro imefanyika leo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Rais John pombe kusafari kwa gari mpaka arusha Leo.
Rais Magufuli leo atasafiri kutoka Dodoma kuelekea Arusha kupitia Mkoa wa Manyara kwa njia ya Barabara.Rais atatumia nafasi kukagua ujenzi wa barabara ya Babati mpaka Dodoma kupitia Barabara kuu ya Kondoa ambayo ni kiunganishi cha mikoa ya Kaskazini na Kusini.Rais pia atatumia muda kuangalia athari za mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika vijiji vilivyoko pembeni mwa barabara ya Dodoma-Arusha.Kuna uwezekano wananchi wa maeneo ya Kondoa, Babati, Monduli, Manyara na Arusha watapata fursa ya kuongea naye ana kwa ana kwa sababu ni kawaida yake kuwasikiliza wananchi moja kwa moja kwa kutumia dhana ya HapaKaziTu.Akiwa Arusha, Rais atahudhuria sherehe za Kijeshi kwa waliohitimu mafunzo ya kijeshi katika chuo cha Kijeshi ambacho kipo wilayani Monduli. Baadaye atafungua Jengo la Mfuko wa PPF katika eneo la Uzunguni. Arusha.
Thursday, May 5, 2016
Mme amchinja MTOTO
Bagamoyo. Mkazi wa Makongo Dar esalaam Oliver Erasto (22) pamoja na mtoto wake Emmanuel Frowin( 3) wameuawa kinyama kwa kuchinjwa shingo na kisha miili yao kutelekezwa kwenye kichaka kilichopo Kaole kata ya Dunda wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mume wa Oliver, Frowin Mbwale (26) mkazi wa Kawe Dar esalaam anadaiwa kufanya mauaji hayo baada ya kumlaghai wakaangalie maendeleo ya ujenzi wa nyumba yao waliyokuwa wameanza kuijenga huko Kaole Bagamoyo na hivyo kwa pamoja na mtoto wao waliongozana kuelekea huko.
Kamanda wa Polisi Pwani Boniveture Mushongi amesema wana familia hao walitumia usafiri wa pikipiki ambayo iliendeshwa na Mbwale.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa Mbwale alishirikiana na rafiki yake aitwaye Rajabu Jumanne (20) mkazi wa Makongo Dar esalaam kuwachinja shingoni mama huyo na mtoto wake.
Kamanda Mushongi amebainisha kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo kusubiri uchunguzi wa daktari na utambuzi wa ndugu.
“Uchunguzi wa awali umebaini mauaji hayo yalitokana na wivu wa mapenzi ambapo mume huyo alikuwa akimtuhumu mda mrefu mkewe huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa yao na mtu aliyetajwa jina moja la Hamza mkazi wa Kawe,” alisema na kuongeza:
“Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari imedaiwa kuwa katika eneo ilikofanyika mauaji imekutwa begi,simu mbili za kiganjani zikiwa na line mbili pamoja na pikipiki ambayo ndiyo iliyokuwa imetumika kwa safari yao kutoka Dar esalaam hadi Bagamoyo siku ya tukio.”
Afisa habari waJeshi la Polisi Pwani Hassan Mtengefu ameongeza kuwa tayari mtuhumiwa huyo mume na rafiki yake Juma wamekamatwa na kwamba walifanikiwa kuwakamata wakiwa njiani kutoroka huko eneo la Zinga Bagamoyo juzi usiku saa 3.30.
" Ni kweli baada ya kupata taarifa kutoka kwa baadhi ya wananchi waliiona miili hiyo porini lakini pia nyayo zao zilionekana kutokana na tope zikielekea vichakani tulikusanya nguvu askari na wananchi walianza msako na tunashukuru tumefanikiwa kuwakata usiku saa 3.30 watuhumiwa hao wakiwa wanataka kutoroka,” alisema
Katika baadhi ya maeneo mjini Bagamoyo yameonekana makundi ya watu hasa wanawake wakijadili tukio hili huku wengi wakiilani na kulitaka jeshi la Polisi pamoja na Mahakama kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa ili iwe fundisho kwa wana familia wengine na walio kwenye mahusiano ya kimapenzi pia.
" Inauma sana jamani, hasa huyu mtoto si malaika huyu, hii si wivu wa kimapenzi bali ni ushetani tuu , wivu gani adi uchinje binadamu mwenzako kinyama vile, si wangeyamaliza tu kifamilia au basi huyo mume angeachana naye tu akatafuta maisha mengine mbona wanawake wapo wengi tu tena wazuri tu, sheria iwawajibishe kisawasawa hawa wanaume" alisema Doris Baton.
TFF yainyang'anya Azam FC,point tatu na kuipa Mbeya city
TFF imechukua maamuzi hayo baada ya azamu kumchezesha mchezaji wake mwenyewe kadi tatu za njoo,baada kupewa mbeya city point tatu azam imeshuka mpaka nafasi ya tatu.
Naibu spika Tulia Ackson amtoa nje ya Mbunge mbuge wa ukonga CHADEMA
Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson leo amewaamuru askari wa Bunge kumtoa Bungeni Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara baada ya mbunge huyo kutaka kumfanyia fujo mbunge wa Kasulu Vijijini Augustine Vuma Holle wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria
Leo Dodoma, Wizara ya Katiba na Sheria ilikuwa ikiwasilisha mpango wa makadirio ya bajeti kwa mwaka 2016/2017 kupitia kwa Waziri wake Harrison Mwakyembe.
Baada ya kuwasilisha kazi ikawa ni zamu ya Wabunge kuchangia bajeti hiyo, lakini hali ikabadilika wakati Mbunge wa Kasulu Vijijini Augustino Hole alivyopata nafasi ya kuchangia akaanza kwa kutoa kauli kuwa ‘Tundu Lissu ana cheti za Milembe‘ kauli ambayo ilionyesha kutowapendeza baadhi ya Wabunge wa kambi ya upinzani.
Ghafla Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara akainuka na kuanza kupiga kelele kuonyesha kutofurahishwa na kauli hiyo kisha kuanza kusimama na kuanza kupiga meza. Naibu Spika Tulia Ackson Mwansasu akamtaka mbunge huyo kukaa chini, Waitara hakuonyesha kutii amri ndipo Naibu Spika akaamulu askari Polisi wa bunge kumtoa nje ya bunge.

MTOTO aliyezaliwa na vidole 31
Hii ni sehemu ya mikono ya mtoto mikono ya mtoto huyo alinyezaliwa nchini jina
Hii ni miguu ya kijana huyo ,taarifa za madactari zinasema kuwa upasuaji Wa mtoro huyo utagharimu dola 200000,sawa na shilingi mil 500,hela za madafu.
kama ni mfwatiliaji Wa siasa za marekani hii ni habari kubwa
Mgombea Wa chama cha republican Ted Cruz ameamua kuachana na kinyang'alo cha kumtafuta mgombea kupitia kwenye chama chake ! Hivi kumfanya mgombea pekee Wa chama hicho kuwa Donald trump kubaki kwenye mbio hizo ,kupitia ukurasa wake Wa Twitter trump amempongea Cruz kwa uamuzi wake huo .
full hotuba ya kambi ya upinzani leo lissu asema rais anavunja sheria
MAONI YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA.
MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU (MB.)
KUHUSU
MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KWA MWAKA 2016/2017
(Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016)
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
Kabla ya kufanya kazi ambayo ninatakiwa kuifanya kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge lako tukufu na ambayo umeniitia, naomba – kwa ridhaa yako – niseme maneno machache juu ya jambo binafsi linalonihusu mimi na familia yangu. Tarehe 7 Aprili, 2016, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Singida katika Bunge la Kumi, Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai, alifariki dunia katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam. Marehemu alikuwa dada yangu na mdogo wangu wa kuzaliwa.
Kufuatia kifo chake, na licha ya kuwa hakuwa Mbunge tena, uongozi wa Bunge lako tukufu ulichukua jukumu la kuhakikisha Marehemu Christina Mughwai anazikwa kwa heshima zote zinazostahili Mbunge. Waheshimiwa Wabunge – kwa namna mbali mbali – walishiriki katika kuhakikisha mpendwa wetu anapata mazishi ya heshima kubwa. Baadhi yenu hata mlifunga safari ya kumsindikiza Marehemu hadi nyumbani kwetu Kijiji cha Mahambe, Wilaya ya Ikungi ambapo mazishi yalifanyika tarehe 13 Aprili, 2016.
Na sio Bunge na Waheshimiwa Wabunge tu. Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano mwenyewe, Dkt. John Pombe Magufuli, ilishiriki moja kwa moja katika mazishi hayo. Licha ya shughuli zake nyingi, Rais mwenyewe alikuja kuupokea mwili wa Marehemu na kutoa heshima zake katika Ukumbi wa kihistoria wa Karimjee. Na baadae kwenye mazishi nyumbani kwetu Mahambe, Rais alimtuma Waziri wake, Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba, kuja kuiwakilisha Serikali katika mazishi hayo. Tulipata kila aina ya msaada tuliohitaji kutoka kwa Bunge, Serikali na Waheshimiwa Wabunge. Hatukuwa wapweke. Hamkutuacha peke yetu katika majonzi yetu. Mlilia na sisi, na mlitufuta machozi. Mlitufariji sana katika kipindi chote cha kilio chetu. Mliufanya msiba wetu kuwa msiba wenu.
Kwa sababu zote hizi, Mheshimiwa Spika, nimetumwa na waliomzaa na kumlea Marehemu Christina Mughwai; nimeagizwa na ndugu zake na marafiki zake na jirani zake, kutoa shukrani zao za dhati kabisa kwa uongozi wa Bunge lako tukufu, kwa Waheshimiwa Wabunge wote na kwa Rais na Mama John Pombe Magufuli na Serikali yake yote, kwa ajili ya wema na upendo na heshima mliyotupatia wakati wa mazishi ya mpendwa wetu Christina Lissu Mughwai. Mwenyezi Mungu awazidishie pale mlikopungukiwa na awabariki sana.
Baada ya kusema haya, Mheshimiwa Spika, sasa naomba nitimize wajibu wangu wa kibunge kama Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu kuhusu hoja iliyoko mezani. Na naomba niweke wazi mapema kwamba nitakayoyasema hapa hayatawafurahisha wengi, ndani na nje ya Ukumbi huu wa Bunge lako tukufu. Hata hivyo, kama alivyosema Frederick Douglass, babu wa harakati za kudai haki za watu weusi wa Marekani ya wakati wa utumwa wa Waafrika zaidi ya miaka mia moja na hamsini iliyopita, “he is a lover of his country who rebukes its sins rather than justify them”, yaani, “ni mpenzi wa nchi yake yule anayekemea madhambi yake badala ya kuyahalalisha.”
UTAWALA BILA SHERIA!
Mheshimiwa Spika,
Tarehe 15 Aprili, 1980, Bunge hili lilitunga Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Kiuwaziri, Sheria Na. 10 ya 1980. Sheria hiyo ilipata ridhaa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na kuanza kutumika Mei Mosi ya 1980. Pamoja na mambo mengine, Sheria hiyo ilimpatia mamlaka ya kuainisha idara, shughuli na mambo mengine ambayo kwayo kazi na majukumu yake amebaki nayo yeye mwenyewe au ameyakasimu kwa Mawaziri na tarehe ya kuanza kutekeleza majukumu hayo.
Tangu wakati huo, imekuwa ni sheria, na sehemu ya mila na desturi ya kikatiba ya nchi yetu, kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kuainisha – kwa kupitia Tangazo lililochapishwa katika Gazeti la Serikali – Wizara, idara, shughuli na mambo mengine ambayo Rais amejibakizia mwenyewe, na yale ambayo amekasimu majukumu yake kwa Mawaziri. Utafiti wetu unaonyesha mambo yafuatayo katika miaka 36 na ya utekelezaji wa Sheria hii:
1. Mwaka 1981, Rais Nyerere alitoa Tangazo la Ukasimishaji wa Majukumu ya Kiuwaziri la mwaka 1981 (The Ministers [Assignment of Ministerial Functions] Notice, 1981, ambalo lilichapishwa katika Gazeti la Serikali kama Tangazo la Serikali Na. 16 la tarehe 6 Februari, 1981;
2. Mwaka 1986, Rais Ali Hassan Mwinyi alitoa Tangazo la Ukasimishaji wa Majukumu ya Kiuwaziri la mwaka 1986 (The Ministers [Assignment of Ministerial Functions] Notice, 1986), ambalo lilichapishwa katika Gazeti la Serikali kama Tangazo la Serikali Na. 29 la 1986;
3. Mwaka 2000, Rais Benjamin William Mkapa alitoa Tangazo la Ukasimishaji wa Majukumu ya Kiuwaziri la mwaka 2000 (The Ministers [Assignment of Ministerial Functions] Notice, 2000), ambalo lilichapishwa katika Gazeti la Serikali kama Tangazo la Serikali Na. 468 la 2000;
4. Mwaka 2006 Rais Jakaya Mrisho Kikwete alitoa Tangazo la Ukasimishaji wa Majukumu ya Kiuwaziri la mwaka 2006 (The Ministers [Assignment of Ministerial Functions] Notice, 2006), ambalo lilichapishwa katika Gazeti la Serikali kama Tangazo la Serikali Na. 2 la tarehe 13 Januari, 2006. Tangazo hilo lilifuta Matangazo mengine yote ya miaka ya nyuma;
5. Mwaka 2010 Rais Kikwete alitoa Tangazo la Ukasimishaji wa Majukumu ya Kiuwaziri la mwaka 2010 (The Ministers [Assignment of Ministerial Functions] Notice, 2010). Tangazo hilo lilichapishwa katika Gazeti la Serikali kama Tangazo la Serikali Na. 494A la tarehe 17 Disemba, 2010. Kama ilivyokuwa kwa Tangazo la mwaka 2006, Tangazo la 2010 lilifuta Matangazo mengine yote yaliyotolewa kabla ya tarehe 17 Disemba, 2010.
Mheshimiwa Spika,
Katikati ya Matangazo haya, Marais waliomtangulia wa nchi yetu Rais Magufuli, katika vipindi tofauti tofauti, wamekuwa wakitumia mamlaka yao chini ya kifungu cha 5(1) cha Sheria, kufanya marekebisho katika majukumu ya kiuwaziri ambayo yalikuwa chini ya Rais mwenyewe, au aliyakasimisha kwa Mawaziri. Hivyo, kwa mfano, mwaka 1982, Mwalimu Nyerere alitoa Tangazo la Serikali Na. 133 la 1982 kwa ajili hiyo. Mwaka 1984, Mwalimu Nyerere alifanya marekebisho mengine kupitia Tangazo la Serikali Na. 210 la 1984.
Aidha, mwaka 1987, Rais Mwinyi alifanya marekebisho kupitia Tangazo la Serikali Na. 206 la tarehe 17 Aprili, 1987. Mwaka uliofuata, Rais Mwinyi alifanya marekebisho mengine kupitia Tangazo la Serikali Na. 42 la tarehe 26 Februari, 1988. Vile vile, mwaka 2003, Rais Mkapa alitoa Tangazo la Serikali Na. 142 la tarehe 16 Mei, 2003. Mwaka huo huo, Rais Mkapa alifanya marekebisho mengine kupitia Tangazo la Serikali Na. 413 la tarehe 19 Disemba, 2003. Aidha, mwaka uliofuata Rais Mkapa alifanya marekebisho mara mbili kupitia Tangazo la Serikali Na. 79 la tarehe 12 Machi, 2004, na Tangazo la Serikali Na. 523 la tarehe 3 Disemba, 2004.
Mheshimiwa Spika,
Tumeelezea jambo hili kwa kirefu kiasi kwa sababu lina umuhimu mkubwa kikatiba na kisheria. Rais hatakiwi kugawa wizara, idara za serikali na majukumu ya kiuwaziri kiholela. Haya ni majukumu ya umma na, kwa sababu hiyo, ni lazima yafanywe kwa kufuata taratibu za kisheria zilizopo. Kwa upande wao, Mawaziri wanatakiwa kutekeleza majukumu waliyokasimiwa na Rais kwa mujibu wa Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Kiuwaziri. Majukumu hayo lazima kwanza yatamkwe, yafafanuliwe na kuainishwa katika Tangazo lililochapishwa kwa ajili hiyo katika Gazeti la Serikali. Ndio maana, kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) cha Sheria hiyo, ushahidi pekee na wa mwisho juu ya suala kama Waziri ana mamlaka katika jambo fulani, ni Tangazo la Rais lililochapishwa chini ya kifungu hicho.
Mheshimiwa Spika,
Kwa sababu ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu inapenda Bunge hili lizifahamu, licha ya mabadiliko makubwa katika, idadi, muundo na majukumu ya Wizara mbali mbali, hadi tunapoandika Maoni haya, Rais Magufuli hajatoa Tangazo lolote juu ya majukumu ya kiuwaziri ambayo yeye mwenyewe amejibakishia na/au yale ambayo ameyakasimu kwa Mawaziri aliowateua. Tofauti na alivyofanya Rais Kikwete na Serikali yake mwaka 2010, hakuna Mbunge hata mmoja ndani ya Ukumbi huu ambaye amepatiwa nakala ya Tangazo lolote lililochapishwa kwa mujibu wa Sheria.
Licha ya madai ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu katika hotuba yake Bungeni ya tarehe 22 Aprili ya mwezi uliopita, Bunge lako tukufu halijapatiwa nakala hata moja inayothibitisha kwamba Mawaziri walioteuliwa na Rais Magufuli, na ambao wamekuwa wakifanya mambo mbali mbali kwa kofia za kiuwaziri, wanatekeleza majukumu waliyokasimishwa kwa mujibu wa Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Kiuwaziri.
Ukweli ni kwamba hata Waziri Mkuu, Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa, amekiri kwamba Serikali inaendeshwa bila kuwa na alichokiita ‘instrument.’ Kwa maneno yake mwenyewe, wakati akifanya majumuisho ya hoja za Wabunge kwa Ofisi yake tarehe 27 Aprili, Waziri Mkuu amesema kwamba “instrument za Wizara zote zimeshakamilika na zimesainiwa (tarehe) 20/04; sasa tunasubiri kutangaza, wakati wowote Mheshimiwa Rais atakapoamua kutangaza zitakuwa zimetoka.” Maana ya kauli hii ni kwamba hakuna instrument yoyote iliyotangazwa kama inavyotakiwa na kifungu cha 5(1) cha Sheria.
Mheshimiwa Spika,
Maana na athari ya kisheria ya kutokuwepo kwa Tangazo la ukasimishaji wa majukumu ya kiuwaziri ni kubwa sana. Wengi wa Mawaziri wa Serikali hii waliteuliwa na Rais Magufuli tarehe 10 Disemba, 2015. ‘Viporo’ vilivyobakia kwenye Baraza la Mawaziri vilikamilishwa tarehe 23 Disemba, 2015. Tangu wakati huo hadi sasa, Mawaziri wamefanya mambo mengi.
‘Wametumbua majipu’ katika Wizara zao na taasisi zilizo chini yake kwa kufukuza, kuachisha, kusimamisha kazi au kuhamisha watendaji na watumishi mbali mbali wa Wizara au taasisi hizo. Wamefanya maamuzi juu ya matumizi ya fedha na rasilmali nyingine za umma.
Yote waliyoyafanya wameyafanya kinyume cha sheria. Hawakuwa na mamlaka ya kufanya waliyoyafanya kwa sababu Mawaziri hawa hawajakasimishwa mamlaka ya utekelezaji wa majukumu yao kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Kiuwaziri. Watendaji na watumishi wote ambao wametumbuliwa majipu na mawaziri hawa wana haki na uwezo wa kwenda mahakamani na kuomba Mahakama zetu zitengue utumbuaji wa majipu waliofanyiwa na Mawaziri wasiokuwa na mamlaka hayo kinyume cha Sheria hii.
Ushauri wangu wa bure kwa watendaji na watumishi hao ni kwamba wakafungue mashauri Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kutumbuliwa kwao majipu na watu wanaojiita Mawaziri lakini hawana hata job description! Kwenda kwao mahakamani sio kutawasaidia kupata haki zao, bali pia kutakomesha vitendo vya kuendesha nchi kienyeji enyeji na bila kufuata sheria, vinavyoelekea kushamiri chini ya utawala huu wa Rais John Pombe Magufuli.
Mheshimiwa Spika,
Kila mtu anafahamu kwamba Rais John Pombe Magufuli sio mwanasheria. Hata hivyo, pamoja na kutokuwa mwanasheria, Rais Magufuli naye anatakiwa kufuata sheria za nchi. Hayuko juu ya sheria. Kiapo chake kinamtaka ‘kuilinda, kuitetea na kuihifadhi’ Katiba ya nchi yetu na sheria zake. Aidha, Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika, kama inavyotamka ibara ya 9(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, “... kuhakikisha ... kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa.”
Kwa sababu Rais Magufuli sio mwanasheria, ameteua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye – kwa maneno ya ibara ya 59(3) ya Katiba – “ndiye mashauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na ... atawajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya kisheria....” Aidha, kwa sababu hiyo hiyo, Rais Magufuli ameteua Waziri wa Katiba na Sheria ili, kama inavyotakiwa na ibara ya 54(3), awe mshauri wake mkuu katika utekelezaji wa madaraka yake katika masuala ya kikatiba na kisheria.
Kwa bahati nzuri, Rais Magufuli amemteua pia Dkt. Harrison George Mwakyembe – mmoja wa wasomi wa juu kabisa wa sheria katika nchi yetu – kuwa Waziri wake wa Katiba na Sheria. Vile vile, Rais Magufuli amemteua Dkt. Sifuni Ernest Mchome – msomi mwingine wa juu kabisa wa sheria – kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria; na Bwana Amon Anastazi Mpanju, mwanasheria mwingine tena, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu inataka kupatiwa majibu sahihi ni kwa nini wanasheria wabobezi wote hawa wameshindwa kumshauri Rais Magufuli kutoa Tangazo la kukasimisha majukumu ya kiuwaziri kwa Mawaziri mbali mbali aliowateua karibu miezi sita iliyopita. Serikali inaendeshwa kama mali binafsi ya Rais Magufuli, bila kufuata wala kuheshimu sheria, sio tu kwa sababu Rais Magufuli ana viashiria vyote vya utawala wa kiimla, bali pia kwa sababu anaelekea kutokuwa na washauri katika masuala ya katiba na sheria za nchi.
Kwa kuangalia mifano ya Matangazo mbali mbali ambayo yametolewa na watangulizi wa Rais Magufuli tangu Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Kiuwaziri ilipotungwa mwaka 1980, hata mwanafunzi wa sheria wa mwaka wa kwanza angeweza kumtengenezea Rais Magufuli draft ya Tangazo la aina hiyo. Iweje watu wenye shahada za uzamivu na uzamili katika sheria washindwe kufanya hivyo kwa karibu nusu mwaka tangu wateuliwe? Kama ni majipu ya kutumbuliwa na Rais Magufuli, basi wasomi hawa wa sheria ni majipu na wanastahili kutumbuliwa. Itatushangaza sana endapo Rais Magufuli atayafumbia macho majipu haya.
UCHAGUZI WA ZANZIBAR NA UKOLONI WA TANGANYIKA
Mheshimiwa Spika,
Sasa naomba nizungumzie masuala ya kikatiba yanayohusu Muungano wetu. Kwa wasiofahamu Katiba yetu na wanaoweza kuhoji kwa nini tunazungumzia masuala ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar katika hoja iliyoko mezani, Sura ya Nne yote ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano inahusu ‘Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (na Rais wa Zanzibar), Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.’ Aidha, ibara ya 104 ya Katiba yetu imewekwa mahsusi kwa ajili ya ‘Uchaguzi wa Kiongozi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.’ Kwa sababu hizi, ni halali kabisa kuzungumzia yaliyotokea Zanzibar katika hoja iliyoko mezani.
Mheshimiwa Spika,
Katika Maoni yake juu ya Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015, Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu – baada ya uchambuzi wa kina wa masuala ya fedha za Muungano - ilisema yafuatayo kuhusu mahusiano kati ya Tanganyika na Zanzibar tangu Muungano wetu uzaliwe tarehe 26 Aprili, 1964:
“Kwa vyovyote vile, takwimu hizi zinaonyesha kwamba, kwa sababu ya Muungano huu, uhusiano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni uhusiano wa kinyonyaji. Kwa sababu hiyo, huu ni uhusiano wa kikoloni. Ni uhusiano kati ya ‘himaya’ ya Tanganyika na ‘koloni’ lake la Zanzibar. Himaya za kikoloni huwa zinadhibiti masuala yote ya ulinzi na usalama, mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa, uraia, kodi, fedha, sarafu na benki kuu ya makoloni yao. Na himaya za kikoloni huwa zinatumia nguvu na udhibiti wao wa masuala haya kuyanyonya makoloni yao kiuchumi, kuyadidimiza kijamii na kuyatawala kisiasa. Hivi ndivyo ambavyo imekuwa kwa mahuasiano kati ya Tanganyika na Zanzibar tangu kuzaliwa kwa Muungano huu tarehe 26 Aprili, 1964.”
Mheshimiwa Spika,
Tangu mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari, 1964, hadi leo hii, Tanganyika imeidhibiti Zanzibar kijeshi na kisiasa. Ukweli ni kwamba – kama ambavyo Harith Ghassany ameonyesha katika kitabu chake Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! Zanzibar na Mapinduzi ya Afrabia – Serikali ya Tanganyika ilishiriki kwa kiasi kikubwa katika maandalizi ya Mapinduzi, ikiwemo kutoa silaha na mafunzo ya kijeshi katika mashamba ya mkonge ya Sakura Estates, Pangani, Tanga, kwa walioipindua Serikali ya Waziri Mkuu Mohamed Shamte na Sultan Jamshid bin Abdullah.
Aidha, siku tatu tu baada ya Mapinduzi hayo, Serikali ya Tanganyika – kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nje na Ulinzi Oscar Salatiel Kambona – ilipeleka vikosi vya Tanganyika Rifles, Jeshi la Tanganyika, ili kuidhibiti Zanzibar kijeshi. Mambo yote haya yamejulikana kwa miaka mingi na wasomi na wanazuoni wa Muungano huu, na yamechapishwa katika vitabu na machapisho mengine rasmi ya kitaaluma ndani na nje ya Tanzania.
Kwa kutumia udhibiti wake wa kijeshi, Tanganyika imedhibiti pia siasa za Zanzibar. Watawala wa Tanganyika ndio wanaoamua nani awe mtawala wa Zanzibar na wamefanya hivyo tangu mwaka 1964. Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi asingekuwa Rais wa Zanzibar baada ya kuuawa kwa Sheikh Abeid Amani Karume mwaka 1972 bila ‘ushawishi’ wa Mwalimu Nyerere na Serikali ya Tanganyika. Na kama ambavyo wanazuoni wa Muungano huu, kama vile Profesa Issa G. Shivji wameonyesha, Jumbe asingeng’olewa madarakani mwaka 1984 bila shinikizo la Mwalimu Nyerere na watu wake hapa Dodoma. Aidha, Rais Mwinyi na Marais wengine wote wa Zanzibar waliomfuatia, ‘wametengenezewa’ Dodoma na sio Zanzibar.
Mheshimiwa Spika,
Tarehe 20 Aprili, 1968, Mwalimu Nyerere alisema yafuatayo wakati akihojiwa na gazeti la The Observer la London, Uingereza: “If the mass of the people of Zanzibar should, without external manipulation, and for some reason of their own, decide that the Union was prejudicial to their existence, I could not bomb them into submission.... The Union would have ceased to exist when the consent of its constituent members was withdrawn.” Yaani, “endapo umma wa wananchi wa Zanzibar wataamua, bila kurubuniwa kutoka nje na kwa sababu zao wenyewe, kwamba Muungano unaathiri kuendelea kuwepo kwao, sitaweza kuwalazimisha kwa kuwapiga mabomu.... Muungano hautaendelea kuwepo pale ridhaa ya washirika wake itakapoondolewa.”
Alichokisema Baba wa Taifa kwamba hatakifanya, Serikali ya Tanganyika imekifanya kwa zaidi ya miaka ishirini sasa. Kabla ya mfumo wa vyama vingi kuruhusiwa mwaka 1992, udhibiti wa Tanganyika kwa siasa za Zanzibar ulifanyika kwa kutumia dhana ya ‘chama kushika hatamu.’ Katika zama za vyama vingi, wananchi wa Zanzibar wamekuwa wapinzani wakubwa wa ukoloni wa Tanganyika kwa nchi yao. Kwa sababu hiyo, tangu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, Serikali ya Tanganyika imetumia mabavu ya kijeshi ya wazi wazi ili kuwaweka madarakani vibaraka wake na kuendelea kuitawala Zanzibar.
Kilele cha matumizi haya ya mabavu ya kijeshi ni Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, ambako vibaraka wa Tanganyika katika Zanzibar walikataliwa kabisa na wananchi wa Zanzibar katika Uchaguzi wa Rais, Wawakilishi na Madiwani. Ni Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) tu ndilo ambalo limehakikisha kwamba vibaraka hawa waliokataliwa na wananchi wao, wanaendelea kubakia madarakani.
Kwa maoni yetu, Mheshimiwa Spika, katika mazingira haya, tatizo la msingi la Zanzibar sio Jecha Salim Jecha wala ZEC wala Ali Mohamed Shein. Hawa ni vibaraka tu wasiokuwa na nguvu wala uhalali wowote. Bila nguvu ya Tanganyika vibaraka hawa hawawezi kudumu madarakani kwa muda mrefu. Tatizo la msingi ni ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar ambao umevikwa joho la Muungano. Bila kulivua joho hili na kushona lingine badala yake, Zanzibar haitakuwa huru na itaendelea kutawaliwa na Tanganyika kisiasa, kiuchumi na kijeshi.
KUNYAMAZISHA UPINZANI NI KUKARIBISHA UDIKTETA!
Mheshimiwa Spika,
Mwanaharakati mmoja wa haki za binadamu wa karne ya 19 aliwahi kuandika kwamba: “Once a government is committed to the principle of silencing the opposition, it has only one way to go, and that is down the path of increasingly repressive measures, until it becomes a source of terror to all its citizens and creates a country where everyone lives in fear”, yaani “pale serikali inapoamua kunyamazisha upinzani, inakuwa na njia moja tu ya kupita, nayo ni njia ya kuongezeka kwa vitendo vya kikandamizaji, mpaka serikali hiyo inakuwa chanzo cha hofu kwa wananchi wake wote na inatengeneza nchi ambapo kila mmoja anaishi kwa hofu.”
Maneno haya yametimia katika nchi yetu. Kwa sababu ya kubaka demokrasia kwa kutumia nguvu za kijeshi Zanzibar ili kukipokonya Chama cha Wananchi (CUF) ushindi wake halali, Serikali hii ya hapa kazi tu imeingia katika njia ya kuongezeka kwa vitendo vya kikandamizaji kila mahali katika nchi yetu. Katika Jiji la Tanga ambako CCM ilikataliwa na wananchi, Serikali hii ilitumia ghilba na mabavu ya kila aina kuhakikisha CCM inanyakua Umeya wa Jiji hilo. Leo viongozi wa vyama vya UKAWA na madiwani waliochaguliwa na wananchi wanakabiliwa na mashtaka ya kutengeneza kwa sababu tu ya kukataa kwao kutawaliwa na watu ambao hawakupata ridhaa ya wananchi.
Hivyo ndivyo ilivyotokea katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, ambako ilibidi Mbunge wa Jimbo la Kilombero na mjumbe halali wa Halmashauri hiyo atolewe kwa nguvu na mapolisi ili kuiwezesha CCM, iliyokataliwa na wananchi kwenye kura, kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya. Sasa Mbunge huyo naye anakabiliwa na mashtaka ya jinai mahakamani kwa kosa la kutetea demokrasia na utawala wa sheria na kukataa utawala wa mabavu na udikteta.
Katika Jiji la Dar es Salaam na Halmashauri zake, licha ya nguvu kubwa na hila nyingi zilizotumiwa na Serikali hii, wananchi wa Dar es Salaam na viongozi wao wa UKAWA walifanikiwa kutetea maamuzi ya wapiga kura na kuzuia jaribio la kubaka demokrasia kwa kuweka Mameya wa chama kilichokataliwa na wananchi kwenye uchaguzi. Hata hivyo, badala ya kuchukua hatua za kijinai dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji, Mwanasheria wa Jiji na Katibu Tawala wa Mkoa waliodiriki hata kugushi hati ya amri ya Mahakama kwa lengo la kuzuia uchaguzi halali wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, leo wanaokabiliwa na mashtaka ya jinai ni Wabunge Halima James Mdee, Saed Ahmed Kubenea na Mwita Mwikwabe Waitara waliohakikisha kwamba uhuni huu wa kisiasa haufanikiwi katika Jiji la Dar es Salaam.
Na sio vyama vya siasa na wanasiasa tu ambao wameangukiwa na adha hii ya Serikali kuingia katika njia ya ukandamizaji. Kwa sababu Rais anatumbua majipu hadharani na, hasa, kwenye vyombo vya habari, sasa Mawaziri nao wanatumbua majipu ya Wizara zao hadharani. Haijalishi kwamba Waziri hawa sio mamlaka ya kinidhamu ya utumishi wa umma na, kama tulivyoonyesha, wala hawajakasimishwa majukumu yoyote kisheria, sasa Mawaziri wanafukuza au kusimamisha au kuhamisha watumishi wa umma walio chini yao.
Wakuu wa Mikoa nao sasa wanatumbua majipu mikoani; wanasimamisha Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa na watumishi wengine wa serikali za mitaa bila kujali kwamba hawana mamlaka yoyote kisheria ya kufanya hivyo. Na siku hizi haipiti wiki moja bila kusikia kwenye vyombo vya habari kwamba Mkuu wa Mkoa au Wilaya fulani ameamuru ameamuru afisa huyu ama yule wa Halmashauri, au diwani huyu au yule, akamatwe kwa sababu hii au ile.
Wote hawa wanafanya hivyo ili wajionyeshe kwamba wanafanya kazi ya Bwana Mkubwa ili asije akawatumbua majipu wao wenyewe. Hofu ya kutumbuliwa majipu ama na Rais mwenyewe ama na Mawaziri ama na Wakuu wake wa Mikoa na Wilaya wake sasa imetanda kila mahali katika utumishi wa umma. Hofu hii inatokana na ukweli kwamba katika kutumbua majipu huku, hakuna tena kufuata utaratibu wa kinidhamu uliowekwa na sheria za nchi yetu. Sasa hatua hizo zinachukuliwa na wasio na mamlaka kisheria katika majukwaa ya kisiasa au kwenye mikutano ya waandishi habari. Na hakuna aliye salama, kuanzia Katibu Mkuu Kiongozi hadi nesi wa hospitalini na mfagizi wa ofisini. Nchi yetu imeingia katika mteremko wenye utelezi mwingi kuelekea kwenye dola la kidikteta.
Mheshimiwa Spika,
Kwa vile Serikali hii ya Rais Magufuli imekumbatia dhana ya kunyamazisha upinzani dhidi yake, uhuru wa vyombo vya habari umewekwa rehani. Kwa kuwa Bunge hili lilijitokeza, katika miaka kumi ya utawala wa Rais Kikwete, kama chombo chenye nguvu ya kuiwajibisha Serikali na watendaji wake, Serikali ya hapa kazi tu imeamua kulinyamazisha na kulifanya kama lilivyokuwa wakati wa miaka ya ‘chama kushika hatamu’, yaani chombo cha kupiga muhuri na kuhalalisha maamuzi ya watawala.
Wala sio siri tena kwamba Kamati za Kudumu za Bunge hili zimepangiwa nje ya Bunge na mamlaka ambazo sio za kikatiba wala kikanuni. Na wala sio siri tena kwamba sasa Bunge hili linaongozwa kwa maagizo ya Ikulu. Ndio maana kila kiongozi wa Bunge sasa anajipendekeza Ikulu kwa vitendo ambavyo mara nyingine vinafedhehesha, kama vile kumpelekea Rais Magufuli fedha zilizoidhinishwa na Bunge hili kwa ajili ya matumizi yake ili zikanunue madawati ya mashule. Kufuta matangazo ya moja kwa moja ya televisheni ni sehemu tu ya mkakati wa kulinyamazisha Bunge ili lisiendelee kuwa chombo cha kuiwajibisha Serikali.
Mkakati wenyewe ni kunyamazisha upinzani dhidi ya utawala huu. Mkakati huu umelenga vile vile kunyamazisha vyombo binafsi vya habari ambavyo wakati mwingine vimekuwa ni sauti ya upinzani kwa watawala wa nchi hii. Ndio maana hata nusu mwaka haikupita na Serikali hii ikaanza kufuta – sio kufungia! - magazeti binafsi yanayotoa habari zisizowapendeza watawala, na kutishia hatua hiyo hiyo kwa magazeti mengine.
Mheshimiwa Spika,
Hata Mahakama ya Tanzania haijapona wimbi hili la ‘kuongezeka kwa vitendo vya kikandamizaji.’ Ibara ya 107A(1) ya Katiba ya nchi yetu inatamka wazi kwamba “mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakama.” Aidha, ibara ya 107B ya Katiba hiyo imeweka wazi kwamba “katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti ya Katiba na yale ya sheria za nchi.”
Licha ya msimamo huu wa kikatiba, Serikali hii ya hapa kazi tu imeanza kuingilia uhuru wa mahakama kwa njia za ajabu, kama sio za kutisha. Kwa mfano, wakati wa sherehe za ufunguzi wa mwaka wa kimahakama mwanzoni mwa mwezi Februari ya mwaka huu, Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), Bwana Charles Rwechungura alitoa mfano wa Mkuu wa Wilaya ya Babati, Crispin TP Meela (mwenyewe mwanasheria na mwanachama wa TLS!) aliyeamuru hakimu mmoja wa Mahakama ya Mwanzo akamatwe na kuwekwa mahabusu baada ya hakimu huyo kutoa hukumu ambayo haikumfurahisha Mkuu wa Wilaya.
Kitendo kama hicho kiliwahi kutokea katika miaka ya 1970 wakati Mkuu wa Mkoa wa Mara alipoamuru watuhumiwa waliopewa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Musoma wakamatwe na kurudishwa rumande. Hakimu Mkazi aliyewapa watuhumiwa hao dhamana alichukua hatua ya kumjulisha Jaji Mkuu, wakati huo Marehemu Francis Lucas Nyalali juu ya kitendo hicho cha Mkuu wa Mkoa. Siku hiyo hiyo taarifa hizo zilimfikia Rais Nyerere na wiki mbili baadae Mkuu wa Mkoa alihamishwa kutoka Mkoa wa Mara. Leo hakimu anakamatwa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya lakini kwa sababu ya hofu iliyotanda ya kutumbuliwa majipu, Jaji Mkuu na Mahakama nzima imenyamaza kimya.
MAJIPU YA MAHAKAMA!
Mheshimiwa Spika,
Sasa naomba nizungumzie masuala ya Mahakama ya Tanzania ambayo, kwa sababu ya utamaduni uliojengeka kwa miaka mingi wa kulindana, hayazungumzwi. Tarehe 30 Novemba, 2014, Bunge hili lilipitisha kwa kauli moja Maazimio ya Bunge Kuhusu Hoja ya Taarifa Maalum ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuhusu Taarifa ya Ukaguzi Maalum Kuhusiana na Miamala Iliyofanyika Katika Akaunti ya ‘Escrow’ ya Tegeta Pamoja na Umiliki wa Kampuni ya IPTL, maarufu kama Maazimio ya Tegeta Escrow Account.
Azimio la 4 la Maazimio ya Tegeta Escrow Escrow lilisema yafuatayo: “KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha kwamba katika watu waliotajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kashfa ya miamala ya Akaunti ya Escrow wapo pia Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania; KWA KUWA, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ... imeweka utaratibu mahsusi wa kushughulikia nidhamu ya Majaji; KWA KUWA, utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji kwa mujibu wa Katiba unamtaka Rais kuunda Tume ya Uchunguzi wa Kijaji kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Majaji; NA KWA KUWA, utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji unamruhusu Rais kumsimamisha kazi Jaji au Majaji husika wakati uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea; HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aunde Tume ya Kijaji ya Uchunguzi kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania.”
Mheshimiwa Spika,
Baada ya Bunge lako tukufu kupitisha maazimio haya, tarehe 22 Disemba, 2014, Rais Jakaya Kikwete aliwahutubia ‘Wazee wa Dar es Salaam’ ambako alisema yafuatayo kuhusu Azimio la Majaji wa Tegeta Escrow: “Azimio hili nimelipokea, (na) tumelijadili. Hata hivyo, itabidi tufuate utaratibu wa kikatiba na kisheria wa kushughulikia masuala ya namna hiyo. Inatakiwa suala kama hili lianzie kwenye Mhimili wa Mahakama yenyewe na siyo kwa Rais au Bunge. Tume ya (Utumishi wa) Mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kumtaka Rais aunde Tume ya Kijaji ya kumchukulia hatua Jaji yeyote pale inapodhihirika kuwa amepoteza sifa za kuendelea kufanya kazi hiyo. Nashauri suala hili tumuachie Jaji Mkuu wa Tanzania alishughulikie atakavyoona inafaa.”
Mheshimiwa Spika,
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari mwaka jana, baada ya maelezo hayo ya Rais Kikwete, Jaji Mkuu, Mheshimiwa Mohamed Chande Othman aliunda jopo la Majaji watatu, chini ya Mwenyekiti wake, Jaji Mbarouk Salim Mbarouk wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania. Aidha, mwishoni mwa mwaka jana, Jaji Mkuu Othman aliwaambia waandishi habari kuwa taarifa ya uchunguzi ya Tume ya Jaji Mbarouk ilikuwa ‘imeiva.’ Cha kushangaza, Mheshimiwa Spika, tangu kuiva kwa taarifa hiyo, Jaji Mkuu Othman, na Serikali hii ya CCM, wamepata kigugumizi kikubwa cha ‘kuipakua’ ili Bunge lako tukufu na Watanzania kwa ujumla ‘waile’! Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu inamtaka mtoa hoja alieleze Bunge lako tukufu iliko taarifa ya uchunguzi wa Majaji wa Tegeta Escrow na kwa nini haijaletwa mbele ya Bunge lako tukufu kwa taarifa au kwa mjadala.
SOMO KUTOKA KENYA
Mheshimiwa Spika,
Hatuna budi kujifunza namna ya kushughulikia masuala ya maadili ya Majaji wetu kutoka kwa jirani zetu. Naomba, katika hili, kutoa mfano wa hivi karibuni kutoka nchini Kenya. Mapema mwaka huu, Jaji Phillip Tunoi wa Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya Kenya alituhumiwa katika kashfa inayofanana na kashfa ya Majaji wa Tegeta Escrow. Mara baada ya tuhuma dhidi ya Jaji Tunoi kutolewa hadharani, Jaji Mkuu wa Kenya, Dkt. Willy Mutunga, aliunda Tume ya Uchunguzi ya Kijaji kuchunguza tuhuma hizo. Mnamo tarehe 5 Februari ya mwaka huu, ndani ya kipindi cha wiki mbili, Jaji Mkuu Mutunga alimkabidhi Rais Uhuru Kenyatta taarifa ya uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Jaji Tunoi.
Kwetu Tanzania ni zaidi ya mwaka na nusu tangu Bunge lako tukufu lipitishe azimio la kuunda Tume ya kuwachunguza Majaji wa Tegeta Escrow na Jaji Mkuu wetu anaelekea kuwa amekalia taarifa ya uchunguzi huo, kama kweli ulifanyika.
Tarehe 12 Februari, 2016, Kamati ya Kudumu ya Fedha za Serikali (PAC) ya Bunge la Kenya ilitoa taarifa iliyomtuhumu Jaji Mkuu Mutunga kuwa hachukui hatua zozote dhidi ya vitendo vya rushwa vinavyofanywa na Majaji, Wasajili na Mahakimu wa Kenya. PAC ya Kenya ilimtaka Jaji Mkuu Mutunga kuwajibika ama kuwajibishwa, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwenye nafasi ya Jaji Mkuu wa Kenya kwa kushindwa kudhibiti maadili ya maafisa hao wa Mahakama ya Kenya.
Siku moja baadae, Jaji Mkuu Mutunga aliijibu PAC kwa kutoa takwimu zilizothibitisha jitihada za Mahakama ya Kenya katika kukabiliana na rushwa na ufisadi ndani ya Mahakama hiyo. Kwa maelezo ya Jaji Mkuu Mutunga, “... three judges have been referred to a tribunal ... on allegations of corruption, a few others are under consideration in the Judicial Service Commission, a Chief Registrar and five Directors have been dismissed, 9 magistrates and 65 Judicial Staff are facing disciplinary proceedings, some have been dismissed or retired in the public interests....”
Kwetu Tanzania, kwa mujibu wa Taarifa ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (MB), Akiwasilisha Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara Kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 mwezi uliopita: “Tume (ya Utumishi wa Mahakama) ilishughulikia jumla ya mashauri 14 ya nidhamu kwa watumishi wa mahakama na kutolewa uamuzi.
Katika hayo watumishi 10 walifukuzwa kazi baada ya kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu na mengine 4 yanafanyiwa uchunguzi zaidi.”
Na kwa kadri ya ufahamu wa Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu, mara ya mwisho Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania aliwahi kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa utovu wa maadili ilikuwa ni mwanzoni kabisa mwa miaka ya 1990, wakati Jaji Mwakibete alipoondolewa na Rais Ali Hassan Mwinyi kwa tuhuma za rushwa na baada ya kuundiwa Tume ya Uchunguzi ya Kijaji. Tangu wakati huo, inaelekea Majaji wa Tanzania wamekuwa malaika na watakatifu wasiokula kula rushwa wala kufanya makosa mengine ya utovu wa maadili, maana hakuna hata mmoja ambaye ameundiwa Tume ya Uchunguzi ya Kijaji au kuchukuliwa hatua stahiki za kinidhamu.
Hii, Mheshimiwa Spika, haiwezi kuwa kweli. Kwa jinsi ambavyo tuhuma za rushwa na ufisadi katika ngazi zote za Mahakama ya Tanzania zimekuwa kubwa na kwa miaka mingi, ni wazi hatuna malaika wala watakatifu katika Mahakama ya Tanzania. Na kwa ushahidi wa Addendum Juu ya Uteuzi wa Majaji niliyoitoa kufuatia Maoni yangu mbele ya Bunge lako tukufu ya tarehe 13 Julai, 2012, matatizo ya utovu wa maadili katika Mahakama zetu za juu ni makubwa sana.
Kwa sababu hiyo, ni lazima sisi kama Bunge na kama taifa tutumbue majibu makubwa na mengi ya Mahakama ya Tanzania. Bunge lako tukufu lisinyamaze kwa hofu ya kuwaudhi Majaji na Mahakimu wetu. Kukosekana kwa haki katika Mahakama zetu kutapelekea machafuko katika nchi yetu. Kama kiongozi maarufu wa Mapinduzi ya Mexico ya 1910, Emiliano Zapata, alivyowahi kusema: “If there is no justice for the people, let there be no peace for the government”, yaani “kama hakuna haki kwa wananchi, basi kusiwe na amani kwa serikali.”
---------------------------------------------------------------
Tundu Antiphas Mughwai Lissu
MSEMAJI & WAZIRI KIVULI, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
MEI 5, 2016

dangote atanjwa kuwa chanzo cha kutumbuliwa kairuki
Wakati aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ametajwa kutenguliwa uteuzi wake kwa kukataa kuchukua mshahara wa Serikali kwa miaka mitatu mfululizo, uchunguzi umebaini kuwa jipu la kusamehe kodi Kampuni ya Saruji ya Dangote ndilo lililomwondoa.
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa mbali na Juliet Kairuki kutochukua mshahara wa Sh 5,000,000 kila mwezi aliopangiwa na Serikali kwa miaka mitatu, kwa maana kuwa ameacha kuchukua wastani wa Sh milioni 180 kwa muda huo, anatuhumiwa kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa wawakezaji bila kufuata utaratibu au sheria za nchi.
“Hili la mshahara ni cha mtoto. Amewadanganya wawekezaji wengi kuwa anaweza kuwapa msamaha wa kodi ya VAT, na sasa Serikali hii ilipoingia madarakani ikasema hana mamlaka hayo. Mwekezaji wa kwanza aliyedanganywa ni Dangote,” anasema mtoa taarifa wetu.
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa Novemba, 2015 Kampuni ya Dangote iliingiza nchini makaa ya mawe tani 35,000 kutoka Afrika Kusini na kutaka makaa haya yasamehewe kodi zote.
“Kwa kweli tulishangaa sana. Kwanza, makaa ya mawe si bidhaa za mtaji (capital) bali ni za matumizi tu (consumables). Vifaa vinavyosamehewa kodi ni zile zinazotumika kuzalisha bidhaa nyingine leo, kesho, mwakani au miaka mitano ijayo na kuendelea, ila makaa ya mawe ukiyachoma yanaisha siku hiyo hiyo, hivyo hii si mtaji.
“Ukiacha hilo, hawa watu wa Dangote wameambiwa wanunue makaa ya mawe kutoka Kiwira au Ngaka, lakini hawataki,” kinasema chanzo chetu na kuongeza kuwa kwa mwaka uliopita, waliagiza tani 2,000 tu za makaa ya mawe kutoka Tancoal kinyume cha makubaliano ya kuongeza ajira nchini.
Afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) amefichua katika uchunguzi huu kuwa kinachoendelea kwenye Kampuni ya Dangote ni balaa. “Hii kampuni tulidhani imekuja hapa kukomboa wananchi, lakini uhalisia siyo.
“Kampuni hii inafanya malipo bila kutoa kodi ya zuio, bidhaa inazoingiza nchini pamoja na nyingine kupata misamaha ya kodi bado inaongeza bei zinakuwa ghali mno kwa maana ya kuongeza gharama za uzalishaji na hivyo kupunguza kiasi cha kodi kinachostahili kulipwa… ni shida,” anasema afisa huyo kwa uchungu.
Kutokana na mkanganyiko huo, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata, ameunda timu ya kufanya ukaguzi maalumu kwa Kampuni ya Dangote ambayo imewakuta na hatia.
“Hiyo bilioni 20 ni uchunguzi wa awali, tunaweza kupata kiasi kikubwa zaidi. Tunawashukuru kwa kuandika habari za ukwepaji kodi, na nakuhakikishia sisi tunafuatilia kila mnachochapisha,” anasema mtoa habari wetu.
Afisa mwingine wa TRA anasema mbinu kubwa inayotumiwa na Dangote na kampuni nyingine ambazo tayari TRA imekwishaibaini mbinu wanazotumia kupunguza faida (Tax Base Erosion), kwa kuingia mikataba yenye gharama kubwa na kampuni walizo na uhusiano nazo kibiashara, kuonesha wametumia gharama kubwa wakati uhalisia wanafanya mbinu za kukwepa kodi.
Akizungumzia sakata hili, Mejena Mkuu Mwandamizi wa Kampuni ya Dangote, Vidya Dixit, amekiri kupokea ankara ya malipo kutoka TRA yenye thamani ya bilioni 20 na akasema: “Wakaguzi wa TRA wako hapa, wamefanya uchunguzi wao, wametuletea madai yao, na sisi tunawasiliana na mshauri wetu wa masuala ya kodi, ikithibitika kuwa tunadaiwa kiasi hicho Dangote ni kampuni kubwa, tutalipa.”
Dixit amesema TRA wamekagua mikataba mbalimbali wanayotumia akina Dangote kuagiza bidhaa na huduma, na wakaja na kiasi hicho, hivyo kwake halioni kama ni tatizo, washauri wao wa masuala ya kodi wakikuta ni kweli watalipa tu. Chanzo chetu kimetueleza kuwa mshauri wao ni Kampuni ya PriceWaterhouseCoopers (PWC) ya Afrika Kusini.
Meneja huyo alijibu pia swali kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TRA) inawadai dola 2,867,400 za Marekani (sawa na Sh bilioni 6.3), kwa kusema: “Mimi sisimamii idara ya uhasibu. Madeni hayo yanaweza kuwapo, ila Dangote ni kampuni kubwa, kama kuna madeni ya aina yoyote tutalipa tu baada ya kujiridhisha kuwa ni madeni halali.”
Kuhusu suala la tani 35,000 za makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini, alisema wao kama Dangote hawapaswi kulaumiwa kwani walifuata taratibu zote: “TIC walitupa sisi msamaha wa kodi, sasa tumezungumza na Waziri wa Fedha akasema TIC hawana mamlaka ya kutoa msamaha wa kodi bila kutangaza kwenye Gazeti la Serikali (GN) na kweli hakukuwapo GN yoyote.
“Sasa hapa tunapata tabu kidogo, idara moja ya Serikali inasema hivi na idara nyingine inasema vile, tunapata shida kidogo,” anasema Dixit. Katika makaa hayo ya mawe pekee ambayo wanatakiwa kuyanunua kutoka nchini, Dangote wanadaiwa wastani wa Sh bilioni 1.1.
Kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kwa kiwanda hicho kuwa kimewageuka wafanyabiashara wadogo na kupendelea wafanyabiashara wakubwa kwa njia ya kuwauzia saruji nyingi na kutowajali wadogo, Dixit anasema wao hawana ubaguzi na ucheleweshaji unaweza kutokea kunapotokea dharura.
Anasema kuna wakati wanaangalia nani ana ghala kubwa la kuhifadhia saruji kiasi gani, ila hiyo haiondoi ukweli kwamba hawabagui yeyote anayetaka kununua na kuuza saruji ya Dangote.
“Ukisema kuna walioshindwa kupata saruji kwa wiki moja au mbili, hilo naweza kukuelewa, lakini miezi miwili, wala asikudanganye mtu. Hilo haliwezekani. Ni kweli kule Lindi tunakotoa chokaa, machimbo yote kwa siku tatu zilizopita yalijaa maji, tukashindwa kupata chokaa, lakini zaidi ya hapo kila mtu anapewa fursa sawa ya kununua saruji bila ubaguzi,” anasema Dixit.
Awali, baadhi ya wafanyabiashara waliilalamikia Kampuni ya Dangote kuwa inauza saruji kwa upendeleo, hali inayowafanya wakose mapato kwani wamekopa mikopo benki na wanaishia kutopata saruji kwa wakati hivyo wanashindwa kulipa hiyo mikopo.
“Kuna mfanyabiashara ameweka kwenye akaunti ya Dangote Sh bilioni 2.5, huyu ndiye anayepewa saruji sisi wengine tunapuuzwa. Watanzania wengi wamekopa benki wastani wa Sh milioni 20, 30 au 50 wanaziweka kwenye kampuni ya Dangote na hawapati hiyo saruji. Hii inatutia hasara mno. Tunataka usawa katika biashara hii,” anasema mmoja wa wafanyabiashara anayedai ameweka Sh milioni 25 kwenye Kampuni ya Dangote, lakini hapatiwi saruji.
Pia, wanalalamikia bei kubwa ya saruji ya Dangote kwani wakati kiwanda kinaanza kujengwa Watanzania walitangaziwa kuwa mfuko mmoja wa saruji ungeuzwa kwa Sh 8,000, lakini sasa bei inafikia Sh 16,000 kwa mikoa kama Mwanza na kwa Dar es Salaam inauzwa kati ya Sh 10,800 na 12,500.
Kamishna Mkuu wa TRA, Kidata, hakuwa tayari kulizungumzia kwa undani suala la Dangote zaidi ya kusema: “Hili suala lipo, tunalifanyia kazi, ni mapema mno kulizungumzia kwa sasa.”
Hata hivyo, afisa mwingine mwandamizi alishangaa kusikia kuwa Dangote bado wanatafuta ushauri wa kisheria kama walipe kodi hiyo au la: “Hawa waliishakwenda hadi kwa Bwana Mkubwa wakakubali kulipa, sasa leo inakuwaje wanatafuta ushauri?” Alihoji afisa huyo.
Alichosema ni kuwa kila mfanyabiashara mkubwa kwa mdogo ajiandae kulipa kodi. “TRA haitaingilia mapato halali ya mfanyabiashara yeyote, ila kwa yeyote anayekwepa kodi hili halitavumiliki. Serikali ya sasa inasema hapa ni kazi tu, hakuna habari ya jina kubwa au dogo. Jipu ni jipu tu, bila kujali ni kubwa au dogo, yote yatakamuliwa tu.”
Source: Jamhuri

ccm ya kanusha uvumi unaoenea kwenye mitandao kuhusu mwenyekiti wake na makada wa chama
Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinatoa taarifa potofu kuhusu mchakato wa Mwenyekiti wa sasa wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti cha uongozi wa CCM kwa Rais John Pombe Magufuli kama ilivyo mila na desturi ya Chama Cha Mapinduzi.
Yamekuwepo madai eti Mwenyekiti amekataa au anachelewesha kukabidhi kijiti.
Habari hiyo sio kweli kabisa na ni kinyume chake, kwani Dkt. Kikwete amekuwa akisisitiza kukabidhi madaraka mapema iwezekanavyo. Kwa ajili hiyo kwenye kikao cha Mei 3, 2016 alikataa kusiongezwe agenda nyingine ambazo zitalazimisha Mkutano Mkuu Maalum kuchelewa kufanyika kwa sababu ya kukamilisha maandalizi ya agenda hizo. Alisisitiza agenda iwe moja tu.
Dhamira ya kufanyika Mkutano Mkuu maalum mwezi Juni, 2016 iko pale pale. Kilichoelezwa kwenye kikao ni kutaka kukamilisha utaratibu wa kupata fedha za kugharamia mkutano huo. Taratibu zikikamilika tarehe itapangwa. Mipango ya kutafuta pesa inaendelea na ikikamilika tarehe itatangazwa.
Tunawataka wana-CCM wasihamanike wala kubabaishwa na taarifa za upotoshaji zinazofanywa na watu wenye nia mbaya na CCM. Hawa ni wale wale ambao wamekuwa wakiiombea mabaya CCM bila ya mafanikio.
Pia tunapenda kukanusha madai ati kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwatahadharisha Wajumbe wa Kamati Kuu kuhusu ukimya wa Ndugu Edward Lowassa. Hakuna wakati wowote kauli kama hiyo aliitoa. Ni uzushi mtupu. Jina la Ndugu Lowassa halikutajwa kabisa.
Aidha, tunapenda kukanusha madai ya kufanyika mkutano baina ya Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa CCM kuhusu uchaguzi wa Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM. Hapajawahi kufanyika mkutano wa aina hiyo siku yoyote na mahali popote. Hivyo madai ya kuwepo kwa tofauti baina ya Viongozi wakuu kuhusu nani achaguliwe kuwa Katibu wa Wabunge wa CCM hayana msingi wowote.
Kamati Kuu iliteua Wabunge wanne kugombea na kuwaachia Wabunge wa CCM kuamua. Kuhusisha Viongozi na hasa kuzua kuwepo kutokuelewana ni jambo la kusikitisha. Ni taarifa ya uongo yenye nia ovu kwa CCM na Viongozi wake.
Tunapenda kuwatahadharisha waandishi wa habari kuandika habari za ukweli. Waache kuzua mambo yenye kupandikiza chuki na mgawanyiko usiostahili kuwepo ndani ya CCM na kuyaeneza kwa watu. Waheshimu maadili ya kazi zao.
Napenda kuwahakikishia na kusisitiza kuwa hakuna mgogoro wa kukabidhi kijiti cha uenyekiti katika CCM na wala hautakuwepo.
Imetolewa na;
Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
05/05/2016

urusi kuimarisha uhusiano na tanzania
baraza la madiwani kinodoni la wasimamisha kazi watumishi watatu
BARAZA la Madiwani Manispaa ya Kinondoni imewasimamisha kazi watumishi wawili akiwemo mwanasheria mkuu wa manispaa hiyo kwa kosa la kuisababishia hasara serikali ya Shilingi Bilioni 7.<br /><br />Hayo yametokea leo, katika waliosimamishwa yupo mwanasheria wa Halmashauri na mfanyakazi mwingine. Kuna upotevu wa pesa nyingi sana na wamesababisha serikali hasara zaidi ya billioni saba.<br /><br />=====================<br /><br />Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Boniface Jacob mapema leo Mei 5.2016 ametangaza kuwasimamisha kazi kwa watumishi wawili wa Manispaa ya Kinondoni, akiweo Mwanasheria Mkuu BW. Burton Mahenge na Mthamini wa Manispaa Bw. Einhard Chidaga baada ya Madiwani kuamua kwa kauli moja kuwachukulia hatua hiyo.<br /><br />Kikao cha Kamati ya fedha na Uongozi cha tarehe 29/04/2016, kiliagiza kuwa yaorodheshwe mashauri yote ambayo hayakusimamiwa vizuri na Mwanasheria wa Manispaa Bwana Burton Mahenge, na hivyo kuisababishia Manispaa kupata hasara, kupoteza mali, na kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.Kufuatia makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo, baraza la Madiwani la terehe 04/05/2016, limeamua kuwasimamisha kazi Mwanasheria Mkuu wa Manispaa Bw. Burton Mahenge, na Mthamini wa Manispaa Bw. Einhard Chidaga.<br /><br />Makosa yaliyogundulika katika Mashauri hayo ni kama yafuatayo:-<br /><br />1. Mradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa.<br />Mkataba huo, ulifanyiwa marekebisho mbalimbali bila idhini ya Halmashauri na hali hiyo kumpatia sauti zaidi Mwekezaji na kuamua analotaka. Manispaa ilipaswa kupata shilingi milioni 900 kwa mwaka katika uwekezaji huo,lakini kutokana na Mgogoro wa kimkataba mapato hayo hayajawahi kulipwa hivyo kupoteza shilingi billion 4.5 mpaka sasa. Mradi ulikamilika tangu 2011 katika viwanja vyote viwili kiwanja Na.277 na 322 ambapo uwekezaji katika kiwanja namba 277 una nyumba (Apartments) 44 na katika kiwanja Na.322 nyumba 68 (Mwekezaji nyumba 29 KMC Nyumba 17)<br /><br />2 .Mgogoro wa wapangaji wa Nyumba za Magomeni Kota.<br />Manispaa iliandaa mpango wa kuendeleza eneo la Magomeni Kota , hivyo kuwaondoa wapangaji hao na kubomoa nyumba hizo kongwe. Wapangaji walifungua shauri la kupinga kuondolewa katika nyumba, na kutoa madai ya kujengewa nyumba,ama kulipwa fedha za fidia kutokana na usimamizi hafifu wa shauri hili Mahakama imeruhusu iliamuru Manispaa kukaana kumalizana na wapangaji nje ya mahakama. <br /><br />Halmashauri ikatengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji kiasi cha shilingi 1,080,000/= kwa kila mpangaji kama kodi ya Mwaka na kumpatia kila mpangaji kiwanja.Hivyo Manispaa inatakiwa kulipa shilingi 3,271,520,000/= kugharamia fidia hiyo,kwa mchanganuo wa Tshs.695,520,000/= pango la mwaka na Tsh2,576,000,000/=fidia ya viwanja 644.<br /><br />3.Uwekezaji Eneo la Coco Beach Oysterbay.<br />Manispaa iliingia Mkataba wa Q-Consult Limited. Kampuni hiyo ilishindwa kutekeleza mradi kwa wakati na Manispaa ikavunja Mkataba huo. Q-consult Limited ilifungua shauri ambalo halikusimamiwa vizuri na kwa sababu ya kutofika kwenye kesi, Manispaa ilipoteza kesi hiyo. <br /><br />Halmashauri iliagiza kukata kwa rufaa lakini hakukuwa na hatua zozote zilizochukuliwa, na hivyo Manispaa inaweza kupoteza haki yake. Iliagizwa na serikali mwanasheria mkuu baada ya tamko la Rais Mhe. John Pombe Magufuli kutangaza nia ya kutoachia eneo hilo mpaka sasa mwanasheria alikuwa hajakata rufaa.<br /><br />4.Mradi wa ujenzi wa maduka Makumbusho (Eastern Capital LTD)<br />Katika shauri hili mabadiliko ya mradi yalifanyika bila idhini ya Halmashauri kwa kubadili michoro na kuongeza maeneo mengine katika mradi kama vile kituo cha Mabasi , Matangazo na choo. viwango vya mgawanyo wa mapato ya Manispaa katika maeneo yaalioongezewa ni kidogo ukilinganisha na uhalisia.<br /><br />Halmashauri haina mkataba na mwekezaji kwa baadhi ya uendeshaji wa majengo 'above two storey'hazipo kwenye kumbukumbu za Halmashauri.<br />Mkataba juu ya ujenzi na uendeshaji wa stendi hauna manufaa kwa Halmashauri ,KMC inapata 1%ya makusanyo kwa mwaka sawa na mil.4 tu kwa mwezi wakati kabla ya uwekezaji ,local standy Halmashauri ilikuwa ikipata 12mil. kwa mwezi.<br /><br />5.Kubomolewa Kwa Ofisi ya Kata ya Msasani.<br />Mwanachi aliyejulikana kwa jina la Chacha aliingilia eneo la Ofisi ya Kata Msasani na baadae kuishitaki Manispaa.Usimamizi dhaifu wa shauri hilo ulisababisha mahakama kutoa amri ya kubomoa ofisi ya Kata, Manispaa imekata rufaa na sasa ni muda mrefu shauri halisikilizwi na hakuna ufuatiliaji unaoendelea. <br /><br />Hata hivyo bwana Chacha kwa makusudi aliamua kuuza kiwanja hiki, kwa Lake Oil Co. Limited wakati shauri halijaisha. Manispaa imekosa manufaa mengi kwa kuchelewa kukamilika kwa shauri hilo.Tangu upandewa pili ulikataa jaji.Tuna zaidi ya mwaka hatuja pangiwa jaji mwingine na hatujafuatilia kama Halmashauri.<br /><br />6.Ujenzi wa Nyumba za Makazi. (Apartments ) Hill Road Oysterbay<br />Mradi unafanyika kwa ubia na Mwekezaji Texas Enterprise company LTD, Mkataba uliingiwa mwaka 2009, na Mradi umesimama kwa Muda Mrefu sasa.<br />Pamefanyika mabadiliko katika Mkataba na Mkataba umefanyiwa marekebisho bila idhini ya Halmashauri. Manispaa inakosa manufaa ya Mali yake kwa sababu ya kuchelewa kwa Mradi. Lakini pia uendeshaji mpya wa sasa hauna makubaliano wa Financial proposal na Investment capital.<br /><br />7. Ujenzi wa nyumba za Makazi(Apartments).Kiwanja Na. 314 Toure Drive.<br />Mradi huu unatekelezwa kwa ubia na Kampuni ya Lake Oil Limited. Mkataba uliingiwa 2019. Mabadiliko yamefanyika katika Mkataba bila Idhini ya Halmashauri na kusababisha Mradi kuchelewa kukamilika.
Lissu awasilisha hotuba ya Waziri kivuli Wa katiba na sheria Leo bungeni
Subscribe to:
Posts (Atom)